Mwanzo › Biblia inasema nini › Faraja
Nyakati ngumu
Biblia inasema nini kuhusu Faraja
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
2 Kor 1:3–4
Na asifiwe Mungu na Baba wa Bwana Yesu Kristo. Yeye ni Baba wa rehema na Mungu wa faraja yote. Mungu hutufariji sisi katika mateso yetu yote, ili kwamba tuweze kuwafariji wale walio katika mateso. Tunawafariji wengine kwa faraja ileile ambayo Mungu alitumia kutufariji sisi.Rum 12:15
Furahini pamoja na wanaofurahi, lieni pamoja na wanaolia.Isa 40:1
''Faraja, faraja watu wangu,'' amesema Mungu.Zab 34:17–18
Wenye haki hulia na Yahwe husikia na kuwaokoa kwenye matatizo yao yote. Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni.Zab 23:4
Hata ijapokuwa nikipita katika bonde la uvuli na giza nene, sitaogopa kudhurika kwa kuwa wewe uko pamoja nami; fimbo yako na gongo lako vya nifariji.Mt 11:28–30
Njoni kwangu, nyinyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo na mtapata pumziko la nafsi zenu. Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.Zab 119:76
Agano lako aminifu na linifariji, kama ulivyomwahidi mtumishi wako.Mt 5:4
Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.Zab 119:50
Hii ni faraja yangu katika mateso: kuwa ahadi yako imeniweka hai.Isa 41:10
Usiogope maana mimi niko pamoja na wewe. Usiwe na wasiwasi, maana mimi ni Mungu wako. Nitakutia nguvu, na nitakusaidia, wewe, na Nitakushika kwa mkono wa haki yangu.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0