Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Maombolezo na kufiwa

Nyakati ngumu

Biblia inasema nini kuhusu Maombolezo na kufiwa

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (14), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Ufu 21:4Atafuta kila chozi kutoka katika macho yao, na hapatakuwa na kifo tena, au kuomboleza, au kulia, au maumivu. Mambo ya zamani yamekwishakupita.
Mt 5:4Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.
Zab 34:18Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni.
Zab 147:3Huponya mioyo iliyopondeka na kuganga majeraha yao.
1 The 4:13Hatutaki ninyi muelewe isivyo sahihi, enyi ndugu, juu ya hao waliolala, ili msije mkahuzunika kama wengine wasio na uhakika kuhusu wakati ujao.
2 Kor 1:3–4Na asifiwe Mungu na Baba wa Bwana Yesu Kristo. Yeye ni Baba wa rehema na Mungu wa faraja yote. Mungu hutufariji sisi katika mateso yetu yote, ili kwamba tuweze kuwafariji wale walio katika mateso. Tunawafariji wengine kwa faraja ileile ambayo Mungu alitumia kutufariji sisi.
Zab 73:26Mwili wangu na moyo wangu huwa dhaifu, bali Mungu ndiye nguvu ya moyo wangu daima.
Yn 16:22Ninyi pia mna huzuni sasa, lakini nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi na hakuna atakayeweza kuiondoa furaha yenu.
Yn 14:27Amani nawapa amani yangu ninyi. Siwapi hii kama ulimwengu utoavyo. Msiifanye mioyo yenu kuwa na mahangaiko, na woga.
Zab 116:15Mauti ya wacha Mungu ina thamani machoni pa Mungu.
Yn 11:25Yesu akamwambia, “Mimi ni ufufuo na uzima; yeye aniaminiye, ingawa atakufa, hata hivyo atakuwa anaishi;
Rum 8:18Kwa kuwa nayahesabu mateso ya wakati huu kuwa si kitu nikilinganisha na utukufu utakaofunuliwa kwetu.
Yn 11:35Yesu akalia.
1 The 4:14Iwapo tunaamini kuwa Yesu alikufa na akafufuka tena, vivyo hivyo Mungu atawaleta pamoja na Yesu hao waliolala mauti katika yeye.

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0