Mwanzo › Biblia inasema nini › Moyo uliovunjika
Nyakati ngumu
Biblia inasema nini kuhusu Moyo uliovunjika
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (13), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Zab 147:3
Huponya mioyo iliyopondeka na kuganga majeraha yao.Zab 34:18
Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni.Ufu 21:4
Atafuta kila chozi kutoka katika macho yao, na hapatakuwa na kifo tena, au kuomboleza, au kulia, au maumivu. Mambo ya zamani yamekwishakupita.Yn 14:27
Amani nawapa amani yangu ninyi. Siwapi hii kama ulimwengu utoavyo. Msiifanye mioyo yenu kuwa na mahangaiko, na woga.Zab 73:26
Mwili wangu na moyo wangu huwa dhaifu, bali Mungu ndiye nguvu ya moyo wangu daima.1 Pet 5:10
Baada ya kuteseka kwa muda kitambo, Mungu wa neema yote, aliyewaita katika utukufu wa milele ndani ya Kristo, atawakamilisha, atawaimarisha na kuwatia nguvu.Zab 55:22
Umtwike mizigo yako Yahwe, naye atakusaidia; yeye hataruhusu mtu mwenye haki kuyumbayumba.2 Kor 4:9
Tunateswa lakini hatujatelekezwa. Twatupwa chini lakini hatuangamizwi.Nah 1:7
Yehova ni mwema, boma katika siku ya taabu; na yeye ni mwaminifu kwa wale wanaomkimbilia.Zab 51:17
Sadaka ya Mungu ni roho iliyovunjika. Wewe, Mungu hautadharau moyo uliopondeka na kujutia.Isa 61:1
Roho ya Bwana Yahwe i juu yangu, maana Yahwe amenipaka mafuta mimi kuhiubiri habari njema kwa wenye taabu. Amenituma mimi kuwaponywa waliopondeka mioyo, kutangaza uhuru kwa wafungwa, na kufungua gereza ili waliofungwa waweze kutoka.Zab 39:12
Sikia maombi yangu, Yahwe, na unisikilize; usikie kilio changu! Usiwe kiziwi kwangu, kwa maana niko kama mgeni pamoja nawe, kimbilio langu la usalama kama mababu zangu walivyokuwa.Mit 12:25
Mashaka katika moyo wa mtu humwelemea, bali neno zuri humfurahisha.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0