Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Mithali 16:9

Mstari wa Biblia · ULB

Mithali 16:9

Katika moyo wake mtu hunuia njia yake, bali Yehova huziongoza hatua zake.

Soma sura nzima: Mithali 16

Katika muktadha

6Kwa agano la uaminifu na udhamini uovu husafishwa na kwa kumcha Yehova watu hujitenga na ubaya.

7Njia za mtu zinapompendeza Yehova, huwafanya hata adui zake huyo mtu wawe na amani naye.

8Bora kitu kidogo pamoja na haki, kuliko mapato makubwa pamoja na udhalimu.

9Katika moyo wake mtu hunuia njia yake, bali Yehova huziongoza hatua zake.

10Mshauri yupo katika midimo ya mfalme, katika hukumu kinywa chake hakisemi kwa udanganyifu.

11Vipimo vya kweli hutoka kwa Yehova; uzito wote kwenye gunia ni kazi yake.

12Wafalme wanapofanya mambo maovu, hicho ni kitu cha kudharauliwa, kwa maana utawala huimarishwa kwa kutenda haki.

Mithali 16

Kwa Kiingereza

Berean Standard BibleProverbs 16:9A man’s heart plans his course, but the LORD determines his steps.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Mit 19:21Moyoni mwa mtu kuna mipango mingi, bali kusudi la Yehova ndilo litakalo simama.
Zab 37:23Hatua za mwanadamu zinaimarishwa na Yahwe, mtu ambaye njia zake zinakubalika machoni pa Mungu.
Mit 16:1Mipango ya moyo ni ya mtu, bali Yehova hutoa jawabu kutoka kwenye ulimi wake.
Mit 20:24Hatua za mtu huongozwa na Yehova; namna gani basi ataifahamu njia yake?
Yer 10:23Ninajua, BWANA, kwamba njia ya mtu haiji kutoka kwake. Wala hakuna mtu atembeaye anayeongoza hatua zake mwenyewe.
Mit 21:30Hakuna hekima, hakuna ufahamu, na hakuna shauri linaloweza kusimama kinyume na Yehova.
Isa 46:10Mimi ninatangaza mwisho kutoka mwanzo, na kabla ya kitu ambacho hakijatokea; Ninasema, ''Mpango wangu utatokea na nitafanya kama ninavyotamani.''

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki