Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Mithali 12:10

Mstari wa Biblia · ULB

Mithali 12:10

Yule atendaye haki anajali mahitaji ya mnyama wake, bali huruma ya mwovu ni ukatili.

Soma sura nzima: Mithali 12

Katika muktadha

7Watu waovu wametupwa na kuondolewa, bali nyumba ya wale watendao haki itasimama.

8Mtu husifiwa kwa kadri ya hekima yake, bali yule anayechagua ukaidi hudharauliwa.

9Bora kuwa na cheo duni- kuwa mtumishi tu- kuliko kujisifu kuhusu ukuu wako bila kuwa na chakula.

10Yule atendaye haki anajali mahitaji ya mnyama wake, bali huruma ya mwovu ni ukatili.

11Yule atendaye kazi katika shamba lake atapata chakula tele, bali anayesaka miradi duni hana akili.

12Watu waovu hutamani wanavyoiba watu wabaya kutoka kwa wengine, bali tunda la wale watendao haki hutoka kwao mwenyewe.

13Mtu mbaya hunaswa kwa maongezi yake mabaya, bali wale watendao haki hujinasua katika taabu.

Mithali 12

Kwa Kiingereza

Berean Standard BibleProverbs 12:10A righteous man regards the life of his animal, but the tender mercies of the wicked are only cruelty.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Kum 25:4Haupaswi kumfunga punda wako pua na mdomo anapokuwa akilima shamba lako.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki