Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Mithali 13:11

Mstari wa Biblia · ULB

Mithali 13:11

Penye majivuno mengi utajiri hufifia, bali yeye apataye pesa kwa kufanya kazi kwa mkono wake pesa zake zitaongezeka.

Soma sura nzima: Mithali 13

Katika muktadha

8Mtu tajiri anaweza kufidia maisha yake kwa mali zake, bali mtu masikini hatapokea kitisho cha aina hiyo.

9Mwanga wa mtu atendaye haki hufurahia, bali taa ya waovu itazimika.

10Kiburi huzaa mafarakano, bali kwa wale wasikiao shauri jema kuna hekima.

11Penye majivuno mengi utajiri hufifia, bali yeye apataye pesa kwa kufanya kazi kwa mkono wake pesa zake zitaongezeka.

12Tumaini linapoachwa, huvunja moyo, bali kukamilishwa kwa shauku ni mti wa uzima.

13Yule ambaye anadharau fundisho bado atakuwa chini ya utawala wake, bali yeye ambaye anaheshimu amri atapewa thawabu.

14Mafundisho ya mtu mwenye hekima ni chemchemi ya uzima, yanakuondoa kutoka kwenye mitego ya mauti.

Mithali 13

Kwa Kiingereza

Berean Standard BibleProverbs 13:11Dishonest wealth will dwindle, but what is earned through hard work will be multiplied.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Mit 20:21Urithi uliopatikana mwanzoni kwa haraka utakuwa na mema kidogo mwishoni.
Mit 10:2Hazina zilizolimbikizwa kwa uovu hakosa thamani, bali kwa kutenda haki hujilinda mbali na kifo.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki