Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › 2 Timotheo 4:3

Mstari wa Biblia · ULB

2 Timotheo 4:3

Kwa maana wakati utakuja ambao watu hawatachukuliana na mafundisho ya kweli. Badala yake, watajitafutia walimu wa kufundisha kulingana na tamaa zao. kwa njia hii masikio yao yatakuwa yametekenywa.

Soma sura nzima: 2 Timotheo 4

Katika muktadha

1Ninakupa agizo hili lenye uzito mbele za Mungu na Kristo Yesu, atakaye wahukumu walio hai na wafu, na kwa sababu ya kufunuliwa kwake na Ufalme wake:

2Hubiri Neno. Uwe tayari kwa wakati ufaao na usiofaa. Waambie watu dhambi zao, kemea, himiza, kwa uvumilivu wote na mafundisho.

3Kwa maana wakati utakuja ambao watu hawatachukuliana na mafundisho ya kweli. Badala yake, watajitafutia walimu wa kufundisha kulingana na tamaa zao. kwa njia hii masikio yao yatakuwa yametekenywa.

4Wataacha kusikiliza mafundisho ya kweli, na kugeukia hadithi.

5Lakini wewe uwe mwaminifu katika mambo yote, vumilia magumu, fanya kazi ya mwinjilisti; timiza huduma yako.

6Kwa maana mimi tayari nimekwisha kumiminwa. Muda wa kuondoka kwangu umewadia.

2 Timotheo 4

Kwa Kiingereza

Berean Standard Bible2 Timothy 4:3For the time will come when men will not tolerate sound doctrine, but with itching ears they will gather around themselves teachers to suit their own desires.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

2 Pet 2:1–3Manabii wa uongo walijitokeza kwa Waisraeli, na walimu wa uongo watakuja pia kwenu. Kwa siri wataleta mafundisho ya uongo nao watamkana Bwana aliyewanunua. Wanajiletea uharibifu wa haraka juu yao wenyewe. Wengi watafuata njia zao za aibu na kupitia wao wataikufuru njia ya ukweli. Kwa uchoyo watawanyonya watu wakitumia maneno ya uongo Hukumu yao haitachelewa, uharibifu utawafuata.
2 Tim 3:1–6Lakini fahamu hili: katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati ngumu. kwa sababu watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye majivuno, wenye dhihaka, wasiotii wazazi wao, wasiokuwa na shukurani na waovu. Wasio na upendo wa asili, wasiotaka kuishi kwa amani na yeyote, wachonganishi, wasingiziaji, wasioweza kujizuia, wenye vurugu, wasiopenda mema. Watakuwa wasaliti, wakaidi, wenye kujipenda wenyewe na wapenda anasa kuliko kumpenda Mungu. Kwa nje watakuwa na sura ya ucha Mungu, lakini wataikana nguvu yake. Jiepushe na watu hao. Kwa kuwa baadhi yao ni wanaume wanaoingia kwenye familia za watu na kushawishi wanawake wajinga. Hawa ni wanawake waliojawa dhambi na wenye kuongozwa na tamaa za kila aina.
1 Tim 4:1–3Sasa Roho anasema waziwazi kwamba katika nyakati zijazo baadhi ya watu wataiacha imani na kuwa makini kusikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya kipepo yatakayofundishwa katika uongo na unafiki. Dhamiri zao zitabadilishwa. Watawazuia kuoa na kupokea vyakula ambavyo Mungu aliviumba vitumiwe kwa shukrani miongoni mwao waaminio na wenye kuijua kweli.
1 Tim 1:10kwa ajili ya waasherati, kwa ajili ya watu wazinzi, kwa ajili ya wale wanaoteka watu na kuwafanya watumwa, kwa ajili ya waongo, kwa ajili ya mashahidi wa uongo, na yeyote aliye kinyume na maelekezo ya uaminifu.
Gal 4:16Hivyo sasa, je nimekuwa adui yenu kwa sababu ninawaambia ukweli?
Yn 3:19–21Hii ndiyo sababu ya hukumu, ya kwamba nuru imekuja ulimwenguni, lakini wanadamu wakapenda giza zaidi ya nuru kwa sababu matendo yao yalikuwa maovu. kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru wala haji nuruni ili matendo yake yasije yakawekwa wazi. Lakini, yeye atendaye kweli huja kwenye nuru ili matendo yake yaonekane kwamba yametendwa kwa utiifu wa Mungu.
Yer 23:16–17Bwana wa majeshi asema hivi, “Usisikilize maneno ya manabii wanaokuhubiri. Wamekudanganya! Wanatangaza maono kutoka kwenye mawazo yao wenyewe, si kwa kinywa cha Bwana. Wanasema daima kwa wale wanaonidharau mimi, 'Bwana asema kutakuwa na amani kwako.' Na kila mtu anayetembea katika ukaidi wa moyo wake anasema, 'mabaya hayatakuja kwenu.'
Yer 6:16–17BWANA asema hivi, 'Simama kwenye njia panda utazame; uliza nzile njia za zamani, 'Je, hii tabia njema iko wapi?' Kisha endelea nayo na tafuta mahali pa kupumzika. Lakini watu wanasema, 'Hatutaenda.' Niliweka walinzi juu yenu ili wasikilize tarumbeta. Lakini walisema, 'Hatutasikiliza.'

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki