Mwanzo › Biblia inasema nini › Kusudi la maisha
Imani
Biblia inasema nini kuhusu Kusudi la maisha
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (12), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Rum 8:28
Nasi twajua ya kuwa kwa wote wampendao Mungu, yeye hufanya mambo yote pamoja kwa wema, kwa wale wote walioitwa kwa kusudi lake.Efe 2:10
Kwa sababu sisi tu kazi ya Mungu, tumeumbwa katika Kristo Yesu kutenda matendo mema. Ni matendo haya ambayo Mungu aliyapanga tangu zamani za kale kwa ajili yetu, ili tutembee katika hayo.Mhu 12:13–14
Mwisho wa jambo baada ya kila kitu umesikika, ni kwamba ni lazima umche Mungu na kushika amri zake, kwa kuwa huu ndilo jukumu lote la mwanadamu. Kwa kuwa Mungu ataleta kila tendo hukumuni, pamoja na kila kitu kilichofichika, kizuri au kibaya.Zab 138:8
Yahwe yuko pamoja nami hadi mwisho; uaminifu wa agano lako, Yahwe, wadumu milele. Usiwaache wale ambao mikono yako imewaumba.Mit 16:9
Katika moyo wake mtu hunuia njia yake, bali Yehova huziongoza hatua zake.1 Pet 2:9
Lakini ninyi ni ukoo uliochaguliwa, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa miliki ya Mungu, ili kwamba mweze kutangaza matendo ya ajabu ya yule aliyewaita kutoka gizani kuja kwenye nuru yake ya ajabu.Rum 12:2
Wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Fanyeni hivi mpate kujua mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yakumpendeza na kamilifu.Yer 1:5
“kabla sijakuumba tumboni, Nilikuchagua; kabla hujazailiwa toka tumboni Nilikutenga; Nilikufanya kuwa nabii kwa mataifa.”Zab 20:4
Naye akujalie haja za moyo wako na kutimiza mipango yako yote.1 Kor 10:31
Kwa hiyo, chochote mnachokula au kunywa, au chochote mfanyacho, fanyeni yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.Zab 37:5
Umkabidhi njia zako Yahwe; uamini katika yeye, naye atatenda kwa niaba yako.Isa 43:7
yeyote aitwe kw jina langu, niliyemuumba kwa utukufu wangu mwenyewe, Niliyemuumba, ndio, Mimi niliyemfanya.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0