Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Mithali 6:16–19

Mstari wa Biblia · ULB

Mithali 6:16–19

16Kuna vitu sita ambavyo Yehova huvichukia, saba ambavyo ni chukizo kwake.

17Macho ya mtu mwenye kiburi, ulimi wa uongo, mikono inayomwaga damu ya watu maasumu,

18moyo unaobuni njama mbaya, miguu inayokimbilia maovu upesi,

19shahidi asemaye uongo na apandaye faraka kati ya ndugu.

Soma sura nzima: Mithali 6

Katika muktadha

13akipepesa macho yake, akiashilia kwa miguu yake na kusonta kwa videle vyake.

14Hufanya njama za uovu kwa hila ya moyo wake; daima huchochea faraka.

15Kwa hiyo msiba wake utamkumba kwa ghafula, punde atavunjika vibaya wala hatapona.

16Kuna vitu sita ambavyo Yehova huvichukia, saba ambavyo ni chukizo kwake.

17Macho ya mtu mwenye kiburi, ulimi wa uongo, mikono inayomwaga damu ya watu maasumu,

18moyo unaobuni njama mbaya, miguu inayokimbilia maovu upesi,

19shahidi asemaye uongo na apandaye faraka kati ya ndugu.

20Mwanangu, itii amri ya baba yako na wala usiyaache mafundisho ya mama yako.

21Uyafunge katika moyo wako siku zote; yafunge kwenye shingo yako.

22utembeapo, yatakuongoza; ulalapo yatakulinda, na uamkapo yatakufundisha.

Mithali 6

Kwa Kiingereza

Berean Standard BibleProverbs 6:16–19There are six things that the LORD hates, seven that are detestable to Him: haughty eyes, a lying tongue, hands that shed innocent blood, a heart that devises wicked schemes, feet that run swiftly to evil, a false witness who gives false testimony, and one who stirs up discord among brothers.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Zab 120:2–3Uiokoe nasfi yangu, yahwe, dhidi ya wale wadanganyao kwa midomo yao na wanenao hila kwa ndimi zao. Yahwe atawaadhibu vipi, na atawafanyia kitu gani zaidi, ninyi mlio na ulimi mdanganyifu?
Zab 11:5Yahweh huwachunguza wote wenye haki na waovu, bali huwachukia wapendao kuwaumiza wengine.
Mit 12:22Yehova anachukia midomo ya uongo, bali wale ambao huishi kwa uaminifu ndiyo furaha yake.
Mit 8:13Hofu ya Mungu ni kuchukia uovu- nachukia majivuno na kiburi, njia ya uovu, na kauli iliyopotoka- hivyo ninavichukia.
Mit 11:20Yehova anawachukia wenye ukaidi mioyoni, bali anawapenda wale ambao njia zao hazina makosa.
Mwa 6:5Yahwe akaona kwamba uovu wa watu umezidi katika nchi, na kwamba mawazo ya mioyo yao daima inaelekea tu katika uovu.
Isa 1:15Hivyo basi mnapotawanya mikono yenu kitkika maombi, sitawangalia hata kama mkiomba sana, sitawasikiliza; mikono yenu imejaa damu.
Mit 1:16miguu ya hukimbilia mabaya na huharakisha kumwaga damu.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki