Bible Explorer Pata programu

Gundua › Njia za safari › Daudi anamkimbia Absalomu

Njia za safari

Daudi anamkimbia Absalomu

Juu ya Mlima wa Mizeituni hadi Mahanaimu, na kurudi kupitia Gilgali · Vituo: 7 · ≈ 130 km kwa mistari iliyonyooka

YerusalemuBahurimuMahanaimuGilgali10 km123456

© OpenStreetMap contributors

Vituo

  1. Yerusalemu2 Sam 15:14Hivyo Daudi akawambia watumishi wake waliokuwa pamoja naye huko Yerusalemu, “Haya na tuinuke na kukimbia kwani hakuna hata mmoja atakayesalimika kwa Absalomu. Jiandaeni kuondoka mara moja asije akatupata mara hata akasababisha madhara juu yetu na kuushambulia mji kwa makali ya upanga.”
  2. Kidroni2 Sam 15:23Nchi yote ikalia kwa sauti kadili watu walivyokuwa wakivuka Bonde la Kidroni, mfalme naye pia akavuka. Watu wote wakasafiri kuelekea nyikani.
  3. Mlima wa Mizeituni2 Sam 15:30Lakini Daudi akaenda bila viatu huku akilia hata Mlima wa Mizeituni, naye alikuwa amefunika kichwa chake. Kila mtu miongoni mwao waliokuwa pamoja naye akafunika kichwa chake, nao wakaenda huku wakilia.
  4. Bahurimu2 Sam 16:5Mfalme Daudi alipokaribia Bahurimu, akaja mtu kutoka katika ukoo wa Sauli, jina lake Shimei mwana wa Gera. Kadiri alivyokuwa akitembea alikuwa akilaani.
  5. Mahanaimu2 Sam 17:24Ndipo Daudi akaja Mahanaimu. Lakini Absalomu yeye akavuka Yordani yeye pamoja na watu wote wa Israeli waliokuwa pamoja naye.
  6. Gilgali2 Sam 19:15Hivyo mfalme akarudi naye akaja Yordani. Na watu wa Yuda wakaja Gilgali kwenda kumlaki mfalme ili kumvusha mfalme juu ya Yordani.
  7. Yerusalemu2 Sam 20:3Daudi alipofika katika kasri lake huko Yerusalemu, akawachukua masuria aliokuwa amewaacha kulitunza kasri, na akawaweka katika nyumba chini ya uangalizi. Aliwaandalia mahitaji yao lakini hakulala nao tena. Hivyo walikuwa wametengwa hadi siku ya kufa kwao, waliishi kama wajane.

Mistari inaunganisha vituo kwa mpangilio wa maandiko. Mahali mstari unafuata ardhi, ndiyo njia inayowezekana kama mtaalamu mmoja alivyoiunda upya; kwingine ni mnyoofu — njia haijulikani. Umbali ni mistari iliyonyooka kati ya vituo. Vistari: kwa meli. Hafifu: mahali hapajulikani kwa hakika.

Kila nukta ni mahali panapowezekana zaidi; nukta hafifu inamaanisha utambulisho hauna uhakika. Mahali pasipojulikana hapapo kwenye ramani.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · UBS Bible Routes, Dr Leen Ritmeyer © United Bible Societies 2023, CC BY-SA 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki