Gundua › Injili kando kwa kando › Katika Yerusalemu
Injili kando kwa kando · Katika Yerusalemu
Kristo ni mwana wa nani?
Mt 22:41–46 · Mk 12:35–37 · Lk 20:41–44
Mt 22:41–4641Na Mafarisayo walipokuwa bado wamejikusanya pamoja, Yesu aliwauliza swali.
42Akisema, “J! e, Mwafikiri nini juu ya Kristo? Yeye ni Mwana wa nani?” Nao wakamjibu, “Ni mwana wa Daudi.”
43Yesu akawajibu, “Ni kwa namna gani Daudi katika Roho anamwita Bwana, akisema,
44'Bwana alimwambia Bwana wangu, “Kaa mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowafanya maadui zako wawekwe chini ya miguu yako.”'?”
45Kama Daudi anamwita Kristo “Bwana,” jinsi gani atakuwa mtoto wake?”
46Hakuna aliyeweza kumjibu neno tena, na hakuna aliyethubutu tena kumwuliza maswali zaidi tangu siku hiyo na kuendelea.
Mk 12:35–3735Na Yesu alijibu, wakati alipokuwa akifundisha katika hekalu, akasema, “Je! waandishi husemaje kuwa Kristo ni mwana wa Daudi?
36Daudi mwenyewe katika Roho Mtakatifu, alisema, 'Bwana alisema kwa Bwana wangu, keti katika mkono wangu wa kuume, mpaka niwafanye maadui wako kuwa chini ya miguu yako.'
37Daudi mwenyewe humwita Kristo, 'Bwana' Je! ni mwana wa Daudi kwa jinsi gani?” Na kusanyiko kuu lilimsikiliza kwa furaha.
Lk 20:41–4441Yesu akawaambia, “Ki vipi watu wanasema kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?
42Maana Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti mkono wa kulia,
43mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako. '
44Daudi anamwita Kristo 'Bwana', basi atakuwaje mwana wa Daudi?”
Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.
Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY