Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Katika Yerusalemu

Injili kando kwa kando · Katika Yerusalemu

Yesu alisafisha hekalu

Mt 21:12–17 · Mk 11:15–19 · Lk 19:45–48 · Yn 2:13–22

Mathayo

Mt 21:12–17

12Kisha Yesu akaingia katika hekalu la Mungu. akawafukuza nje wote waliokuwa wakinunua na kuuza hekaluni. Pia alipindua meza za wabadilishaji wa fedha na viti vya wauza njiwa.

13Akawaambia, “Imeandikwa, 'Nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi, 'lakini ninyi mmeifanya pango la wanyang'anyi.”

14kisha vipofu na vilema wakamjia hekaluni, naye akawaponya.

15Lakini wakati wakuu wa makuhani na waandishi walipoona maajabu aliyoyatenda, na waliposikia watoto wakipiga kelele hekaluni na kusema, “Hosana kwa Mwana wa Daudi,” walishikwa na hasira.

16Wakamwambia, “Umesikia kile kinachosemwa na hawa watu?” Yesu akawaambia, “Ndiyo! Lakini hamjawahi kusoma, 'Kutoka kwa midomo ya watoto na watoto wachanga wanyonyao mna sifa kamili?''

17Kisha Yesu akawaacha na kwenda nje ya mji katika Bethania na kulala huko.

Marko

Mk 11:15–19

15Walikuja Yerusalemu, naye aliingia hekaluni na kuanza kuwatoa nje wauzaji na wanunuzi ndani ya hekalu. Alizipindua meza za wabadilishaji wa fedha na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa.

16Hakumruhusu yeyote kubeba chochote hekaluni kilichoweza kuuzwa.

17Aliwafundisha na akasema, “Je haikuandikwa, 'nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote'? Lakini mmeifanya pango la wanyang'anyi”.

18Makuhani wakuu na waandishi walisikia alivyokuwa amesema, nao walitafuta njia ya kumwua. Hata hivyo walimwogopa kwa sababu umati ulishangazwa na mafundisho yake.

19Na kila wakati jioni ilipofika, waliondoka mjini.

Luka

Lk 19:45–48

45Yesu aliingia Hekaluni, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza,

46akiwaambia, “Imeandikwa, 'Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala,' lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi”.

47Kwa hiyo, Yesu alikuwa akifundisha kila siku hekaluni. Makuhani wakuu na walimu wa Sheria na viongozi wa watu walitaka kumuua,

48lakini hawakuweza kupata njia ya kufanya hivyo, kwa sababu watu wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini.

Yohana

Yn 2:13–22

13Basi Pasaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia, hivyo Yesu akaenda Yerusalemu.

14Akawakuta wauzaji wa ng'ombe, kondoo, na njiwa ndani ya Hekalu. Pia na wabadilisha fedha walikuwa wameketi ndani ya Hekalu.

15Yesu akatengeneza mjeledi wenye vifundo, akawatoa wote walikuwemo katika hekalu, ikijumuisha ng'ombe na kondoo. Akamwaga fedha za wabadili fedha na kuzipindua meza zao.

16Kwa wauzaji wa njiwa akawambia, “Toeni vitu hivi mbali na mahali hapa, acheni kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa mahali pa soko.”

17Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa ilikuwa imeandikwa, “Wivu wa nyumba yako utanila.”

18Wakuu wa Kiyahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara ipi utakayoionyesha kwa sababu unayafanya mambo haya?”

19Yesu akawajibu, libomoeni Hekalu hili nami nitalijenga baada ya siku tatu.”

20Kisha wakuu wa Wayahudi wakasema, “Iligharimu miaka arobaini na sita kujenga hekalu hili nawe unasema utalijenga kwa siku tatu?”

21Ingawa, yeye aliongea hekalu akimaanisha mwili wake.

22Hivyo baadaye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka kuwa alisema hivyo, wakaamini maandiko na kauli hii ambayo Yesu alikuwa amekwisha kuisema.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY