1Ndipo Mafarisayo na waadishi walikuja kwa Yesu kutoka Yerusalemu. Na kusema,
2“Kwa nini wanafunzi wanayahalifu mapokeo ya wazee? Kwa kuwa hawanawi mikono yao wanapokuwa wanakula chakula.''
3Yesu akawajibu na kuwaambia, “Nanyi—kwa nini mnaihalifu sheria ya Bwana kwa ajili ya mapokeo yenu?
4Kwa kuwa Mungu alisema, 'Mheshimu baba yako na mama yako; na 'Asemaye uovu kwa baba yake na mama yake, hakika atakufa.'
5Lakini ninyi husema, 'Kila amwambiaye baba yake na mama yake, '“Kila msaada ambao angepata kutoka kwangu sasa ni zawadi kutoka kwa Mungu,'''
6“Mtu huyo hana haja ya kumuheshimu baba yake. Katika namna hii mmelitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.
7Enyi wanafiki, ni vema kama Isaya alivyo tabiri juu yenu aliposema,
8'Watu hawa wananiheshimu mimi kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami.
9Wananiabudu bure, kwa sababu wanafundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.”'
10Ndipo akawaita makutano na kuwaambia,” Sikilizeni na mfahamu
11Hakuna kitu kiingiacho mdomoni mwa mtu na kumfanya najisi. Bali, kile kitokacho kinywani, hiki ndicho kimfanyacho mtu kuwa najisi.''
12Ndipo wanafunzi wakamwendea na kusema na Yesu, “Je!, Unafahamu Mafarisayo walipolisikia lile neno walikwazika?”
13Yesu aliwajibu na kusema, “Kila mmea ambao Baba yangu wa mbinguni hajaupanda utang'olewa.
14Waacheni pekee, wao ni viongozi vipofu. Kama mtu kipofu atamuongoza kipofu mwenzake, wote wawili wataanguka shimoni.”
15Petro akajibu na kumwambia Yesu,” Tuelezee mfano huu kwetu,
16Yesu akajibu, ''Nanyi pia bado hamuelewi?
17Ninyi hamuoni kuwa kila kiendacho mdomoni hupitia tumboni na kwenda chooni?.
18Lakini vitu vyote vitokavyo mdomoni hutoka ndani ya moyo. Ndivyo vitu vimtiavyo mtu unajisi.
19Kwa kuwa katika moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushuhuda wa uongo, na matusi.
20Haya ndiyo mambo yamtiayo mtu unajisi. Lakini kula bila kunawa mikono hakumfanyi mtu kuwa najisi.”