Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Mafundisho

Injili kando kwa kando · Mafundisho

Heri

Mt 5:1–12 · Lk 6:20–23

Mathayo

Mt 5:1–12

1Yesu alipo uona umati, akaondoka na kuelekea Mlimani. Alipokuwa ameketi chini, wanafunzi wake wakaja kwake.

2Akafunua kinywa chake na akawafundisha, akisema,

3“Heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao.

4Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.

5Heri wenye upole, maana watairithi nchi.

6Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa.

7Heri wenye rehema maana hao watapata Rehema.

8Heri wenye moyo safi maana watamwona Mungu.

9Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.

10Heri wale wanaoteswa kwa ajili ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao.

11Heri ninyi ambao watu watawatukana na kuwatesa, au kusema kila aina ya ubaya dhidi yenu kwa uongo kwa ajili yangu.

12Furahini na kushangilia, maana thawabu yenu ni kubwa juu mbinguni. Kwa kuwa hivi ndivyo watu walivyo watesa manabii walioishi kabla yenu.

Luka

Lk 6:20–23

20Kisha akawaangalia wanafunzi wake, na kusema, “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, kwa maana ufalme wa Mungu ni wenu.

21Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa maana mtashibishwa. Mmebarikiwa ninyi mliao sasa, kwa maana mtacheka.

22Mmebarikiwa ninyi ambao watu watakapowachukia na kuwatenga na kuwashutumu ninyi kwamba ni waovu, kwa ajili ya Mwana Adamu.

23Furahini katika siku hiyo na kurukaruka kwa furaha, kwa sababu hakika mtakuwa na thawabu kubwa mbinguni, kwa maana baba zao waliwatendea vivyohivyo manabii.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY