15Sasa katika sikukuu ilikuwa desturi ya liwali kumfungua mfungwa mmoja anayechaguliwa na umati.
16Wakati huo walikuwa na mfungwa sugu jina lake Baraba.
17Hivyo wakati walipokuwa wamekusanyika pamoja, Pilato aliwauliza, “Ni nani mnataka tumfungue kwa ajili yenu?” Baraba au Yesu anayeitwa Kristo?”
18Kwa sababu alijua kwamba wamekwisha kumkamata kwa sababu ya chuki.
19Wakati alipokuwa akiketi kwenye kiti chake cha hukumu, mke wake alimtumia neno na kusema, “Usitende jambo lolote kwa mtu huyo asiye na hatia. Kwani nimeteswa mno hata leo katika ndoto kwa sababu yake.”
20Ndipo wakuu wa makuhani na wazee waliwashawishi makutano wamwombe Baraba, na Yesu auawe.
21Liwali aliwauliza, “Ni yupi kati ya wawili mnataka mimi nimwachie kwenu?” Walisema, “Baraba.”
22Pilato akawaambia, “Nimtendee nini Yesu anayeitwa Kristo?” Wote wakajibu, “Msulibishe”
23Naye akasema, “Kwa nini, ni kosa gani ametenda?” Lakini walizidi kupaza sauti hata juu mno, “Msulibishe.”
24Hivyo wakati Pilato alipoona hawezi kufanya lolote, lakini badala yake vurugu zilikuwa zimeanza, alitwaa maji akanawa mikono yake mbele ya umati, na kusema, “Mimi sina hatia juu ya damu ya mtu huyu asiye na hatia. Yaangalieni haya wenyewe.”
25Watu wote wakasema, “Damu yake iwe juu yetu na watoto wetu.”
26Kisha akamfungulia Baraba kwao, lakini alimpiga mijeredi Yesu na kumkabidhi kwao kwenda kusulibiwa.