28Kisha wakamchukua Yesu toka kwa Kayafa mpaka kwenye Praitorio. Ilikwa asubuhi na mapema. Wao wenyewe hawakuiingia ile Praitorio ili wasije wakanajisika na kuila pasaka.
29Kwa hiyo Pilato akawaendea akisema. “Ni shitaka gani linalomhusu huyu mtu?”
30Wakamjibu na kumwambia, “Kama huyu mtu asingekuwa mtenda maovu, tusingemleta kwako.”
31Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi wenyewe, mkamhukumu kulingana na sheria yenu.” Nao Wayahudi wakamwambia, “Sheria haituruhusu sisi kumwua mtu yeyote.”
32Walisema haya ili neno la Yesu litimilike, neno ambalo alikuwa amekwisha sema juu ya aina ya kifo chake.
33Basi Pilato akaingia tena Praitorio akumwita Yesu; akamwambia, “Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?”
34Yesu akamjibu, “Je, wewe waniuliza swali hili kwa Sababu wataka kujua au kwa sababu wengine wamekutuma ili uniulize mimi?”
35Naye Pilato akamjibu, “Mimi si Myahudi, au sivyo?” Taifa lako na kuhani mkuu ndio waliokuleta kwangu; wewe umefanya nini?
36Yesu akajibu; “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu, kama ufalme wangu ungekuwa na sehemu katika ulimwengu huu watumwa wangu wangenipigania ili nisitolewe kwa wayahudi. Kwa kweli ufalme wangu hautoki hapa” Basi
37Pilato akamwambia, “Je, wewe basi u mfalme?” Yesu akajibu, “wewe ndivyo unanvyosema kuwa mimi ni mfalme, Kwa sababu hii mimi nilizaliwa na kwa sababu hii mimi nimekuja ulimwenguni ili niwe shahidi wa ile kweli. Yeyote aliye wa hiyo kweli huisikiliza sauti yangu.
38Pilato akamwambia, “Kweli ni nini?” Naye alipokwisha sema haya akaenda kwa Wayahudi na kuwaambia “Siona katika lolote mtu huyu.