Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Mateso

Injili kando kwa kando · Mateso

Askari wamdhihaki Yesu

Mt 27:27–31 · Mk 15:16–20 · Yn 19:2–3

Mathayo

Mt 27:27–31

27Kisha askari wa liwali wakamchukua Yesu mpaka Praitorio na kundi kubwa la maaskari wote wakamkusanyika.

28Wakamvua nguo zake na kumvika kanzu ya rangi nyekundu.

29Kisha wakatengeneza taji ya miiba na kuiweka juu ya kichwa chake, na walimwekea mwanzi katika mkono wake wa kuume. Walipiga magoti mbele yake na kumkejeri, wakisema, “Salamu, Mfalme wa Wayahudi?”

30Na walimtemea mate, na walitwaa mwanzi na kumpiga kichwani.

31Wakati walipokuwa wakimkejeri, walimvua ile kanzu na kumvika nguo zake, na kumwongoza kwenda kumsulibisha.

Marko

Mk 15:16–20

16Askari walimwongoza hadi ndani ya ua (ule ulio ndani ya kambi) na walikusanyika pamoja kikosi cha askari.

17Wakamvika Yesu kanzu ya rangi ya zambarau, na wakasokota taji ya miiba wakamvika.

18Wakaanza kumdhihaki na kusema, “Salam, Mfalme wa Wayahudi!”

19Wakampiga kichwani kwa mwanzi na kumtemea mate. Wakapiga magoti mbele yake kwa kumheshimu.

20Hata wakiisha kumdhihaki, wakamvua ile kanzu ya rangi ya zambarau na kumvika mavazi yake, na wakamtoa nje kwenda kumsulibisha.

Yohana

Yn 19:2–3

2Wale maaskari wakasokota miiba na kutengeneza taji. Wakaiweka juu ya kichwa cha Yesu na kumvalisha vazi la rangi ya zambarau.

3Wakamjia na kusema, “Wewe mfalme wa Wayahudi! na kisha kumpiga kwa mikono yao.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY