Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › 2 Wakorintho 10:5
Mstari wa Biblia · ULB
2 Wakorintho 10:5
Pia, tunaharibu kila chenye mamlaka kijiinuacho dhidi ya maarifa ya Mungu. Tunalifanya mateka kila wazo katika utii kwa Kristo.
Soma sura nzima: 2 Wakorintho 10
Katika muktadha
2Nawaomba ninyi kwamba, wakati nikiwepo pamoja nanyi, sitahitaji kuwa jasiri na kujiamini kwangu mwenyewe. Lakini nafikiri nitahitaji kuwa jasiri wakati nikiwapinga wale wanaodhani kwamba tunaishi kwa jinsi ya mwili.
3Kwa kuwa hata kama tunatembea katika mwili, hatupigani vita kwa jinsi ya mwili.
4Kwa kuwa silaha tunazotumia kupigana si za kimwili. Badala yake, zina nguvu ya kiungu ya kuharibu ngome. Zinaondosha kabisa mijadara inayopotosha.
5Pia, tunaharibu kila chenye mamlaka kijiinuacho dhidi ya maarifa ya Mungu. Tunalifanya mateka kila wazo katika utii kwa Kristo.
6Na tunapata utayari wa kuadhibu kila matendo lisilo na utii, mara tu utii wenu unapokuwa kamili.
7Tazama kile kilichowazi mbele yenu. Kama yeyote anashawishika kwamba yeye ni wa Kristo, na hebu ajikumbushe yeye mwenyewe kwamba kama tu alivyo ni wa Kristo, hivyo ndiyo na sisi pia tuko hivyo.
8Kwa kuwa hata nikijivuna kidogo zaidi kuhusu mamlaka yetu, ambayo Bwana aliyatoa kwa ajili yetu kuwajenga ninyi na siyo kuwaharibu, sitaona haya.
Kwa Kiingereza
We tear down arguments and every presumption set up against the knowledge of God; and we take captive every thought to make it obedient to Christ.Marejeo mtambuka
Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.
Kwa maana neno la Mungu li hai na lina nguvu na linaukali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili. Na huchoma hata kufikia kugawanya nafsi na roho, na viungo kutika uboho. Na lenye kuweza kufahamu fikira za moyo nia yake.Tuwaache waovu waziache njia zao, na mtu mwenye dhambi mawazo yake. Muache yeye arudi kwa Yahwe, na atamuhurumia yeye, na kwa Mungu wetu, yeye ambaye atamsamehe huyo kwa wingi.Kama watoto watiifu, msifungwe wenyewe na tamaa ambazo mlizifuata wakati mlipokua hamna ufahamu. Lakini kama vile aliyewaita alivyo mtakatifu, nanyi, pia, muwe watakatifu katika tabia yenu yote maishani.Lakini naona kanuni iliyo tofauti katika viungo vya mwili wangu. Inapiga vita dhidi ya kanuni mpya katika akili zangu. Inanifanya mimi mateka kwa kanuni ya dhambi iliyo katika viungo vya mwili wangu.Kwa kuwa katika moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushuhuda wa uongo, na matusi.Hii ni kwa sababu, ingawa walijua kuhusu Mungu, hawakumtukuza yeye kama Mungu, wala hawakumpa shukrani. Badala yake, wamekuwa wapumbavu katika mawazo yao, na mioyo yao yenye ujinga ilitiwa giza.Itakaseni mioyo yenu kutoka uovu wenu, Yerusalemu, ili kwamba muokolewe. Mawazo yako mabaya yatafikiri juu ya kutenda dhambi mpaka lini?Kwa kuwa hekima ya dunia hii ni ujinga mbele za Mungu, Kwa kuwa imeandikwa, “Huwanasa wenye hekima kwa hila zao”Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki