Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Waefeso 4:26–27

Mstari wa Biblia · ULB

Waefeso 4:26–27

26Mwe na hasira, lakini msitende dhambi.” Jua lisizame mkiwa katika hasira zenu.

27Msimpe Ibilisi nafasi.

Soma sura nzima: Waefeso 4

Katika muktadha

23Vueni utu wenu wa zamani ili kwamba mfanywe upya katika roho ya akili zenu.

24Fanyeni hivi ili muweze kuvaa utu mpya, unaoendana na Mungu. Umeumbwa katika haki na utakatifu wa kweli.

25Kwa hiyo, weka mbali udanganyifu. “Ongeeni ukweli, kila mmoja na jirani yake,” kwa sababu tu washirika kwa kila mmoja kwa mwenzake.

26Mwe na hasira, lakini msitende dhambi.” Jua lisizame mkiwa katika hasira zenu.

27Msimpe Ibilisi nafasi.

28Yeyote aibaye lazima asiibe tena. Badala yake ni lazima afanye kazi. Afanye kazi yenye manufaa kwa mikono yake, ili kwamba aweze kumhudumia mtu aliye na hitaji.

29Kauli mbaya isitoke kinywani mwenu. Badala yake, maneno lazima yatoke katika vinywa vyenu yafaayo kwa mahitaji, kuwapa faida wale wanaosikiliza.

30Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu. Ni kwa Yeye kwamba mmewekewa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi.

Waefeso 4

Kwa Kiingereza

Berean Standard BibleEphesians 4:26–27“Be angry, yet do not sin.” Do not let the sun set upon your anger, and do not give the devil a foothold.

Nukuu kutoka Agano la Kale

Zab 4:4Tetemekeni na kuogopa, lakini msitende dhambi! Tafakarini mioyoni mwenu kwenye vitanda vyenu na muwe kimya.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Yak 1:19Mnajua hili, ndugu zangu wapendwa. Kila mmoja anapaswa kuwa mwepesi wa kusikia, siyo mwepesi wa kuongea wala kukasirika,
Zab 37:8Usikasilile na kugadhabika. Usiogope. Hii huleta matatizo tu.
Efe 4:31–32Lazima muweke mbali uchungu wote, ghadhabu, hasira, ugomvi, na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. Iweni wema ninyi kwa ninyi. Mwe na huruma. Msameheane ninyi kwa ninyi, kama vile Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Yak 4:7Hivyo, jitoeni kwa Mungu. Mpingeni ibilisi na yeye atakimbia kutoka kwenu.
Mhu 7:9Usikasirike haraka rohoni mwako, kwa sababu hasira hukaa katika mioyo ya wapumbavu.
Mit 14:29Mtu mvumilivu anaufahamu mkubwa, bali mtu mwepesi wa kuhamaki hukuza upuuzi.
Mit 19:11Busara humfanya mtu achelewe kukasirika na utukufu wake ni kusamehe kosa.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki