Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Waefeso 5:18

Mstari wa Biblia · ULB

Waefeso 5:18

Msilewe kwa mvinyo, huongoza kwenye uharibifu, badala yake mjazwe na Roho Mtakatifu.

Soma sura nzima: Waefeso 5

Katika muktadha

15Hivyo iweni makini jinsi mtembeavyo, siyo kama watu wasio werevu bali kama werevu.

16Ukomboeni muda kwa kuwa siku ni za uovu.

17Msiwe wajinga, badala yake, fahamuni nini mapenzi ya Bwana.

18Msilewe kwa mvinyo, huongoza kwenye uharibifu, badala yake mjazwe na Roho Mtakatifu.

19Zungumzeni na kila mmoja wenu kwa zaburi, na sifa, na nyimbo za rohoni. Imbeni na sifuni kwa moyo kwa Bwana.

20Daima toa shukrani kwa mambo yote katika jina la Kristo Yesu Bwana wetu kwa Mungu Baba.

21Jitoeni wenyewe kila mmoja kwa mwingine kwa heshima ya Kristo.

Waefeso 5

Kwa Kiingereza

Berean Standard BibleEphesians 5:18Do not get drunk on wine, which leads to reckless indiscretion. Instead, be filled with the Spirit.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Lk 1:15Kwa kuwa atakuwa mkuu mbele ya macho ya Bwana. Hatakunywa divai au kinywaji kikali, na atakuwa amejazwa na Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake.
Mit 20:1Divai ni dhihaka na kinywaji kikali ni mgomvi; anayepotea kwa kunywa hana busara.
Rum 13:13Na tuenende sawa sawa, kama katika nuru, si kwa sherehe za uovu au ulevi. Na tusienende katika zinaa au tamaa isiyoweza kudhibitiwa, na si katika fitina au wivu.
Gal 5:21–25wivu, ulevi, ulafi na mambo mengine kama haya. Nawaonya ninyi, kama nilivyowaonya mwanzoni, kwamba wale wanaofanya mambo kama hayo hawataurithi ufalme wa Mungu. Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani, upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo. Wale walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na shauku na tamaa zao mbaya. Kama tukiishi kwa Roho, pia tutembee kwa Roho.
Mdo 11:24Kwa sababu alikuwa mtu mwema na amejazwa na Roho Mtakatifu na imani na watu wengi wakaongezeka katika Bwana.
Isa 5:22Ole wao ambao ni washindi kwa kunjwa mvinyo, na wazoefu wa kuchanganya pombe kali;
1 Kor 5:11Lakini sasa nawaandikia kutojichanganya na yeyote anayeitwa kaka au dada katika Kristo, lakini anaishi katika uzinzi au ambaye ni mwenye kutamani, au mnyang'anyi, au mwabudu sanamu, au mtukanaji au mlevi. Wala msile naye mtu wa namna ile.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki