Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › 3 Yohana 1:2
Mstari wa Biblia · ULB
3 Yohana 1:2
Mpendwa, nakuombea ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema, kama vile roho yako inavyofanikiwa.
Katika muktadha
1Mzee, kwa Gayo mpenzi, ninayempenda katika kweli.
2Mpendwa, nakuombea ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema, kama vile roho yako inavyofanikiwa.
3Maana nilifurahi sana wakati nilipoambiwa na ndugu waliokuja na kutoa ushuhuda juu ya kweli yako, kama vile unavyoenenda katika kweli.
4Sina furaha kubwa zaidi ya hii, kusikia kwamba watoto wangu wanatembea katika kweli.
5Mpendwa, unaenenda kwa uaminifu unapowahudumia ndugu na wageni,
Kwa Kiingereza
Beloved, I pray that in every way you may prosper and enjoy good health, as your soul also prospers.Marejeo mtambuka
Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.
Lakini mkue katika neema na ufahamu wa Bwana na mwokozi Yesu Kristo. Na sasa utukufu una yeye sasa na milele. Amina.Tumesikia imani yenu katika Yesu Kristo na upendo mlionao kwa wale wote waliotengwa kwa ajili ya Mungu. Mna upendo huu kwa sababu ya taraja la uhakika lililohifadhiwa mbinguni kwa ajili yenu. Mlisikia kuhusu taraja hiyo ya uhakika kabla katika neno la kweli, injili, ambayo imekuja kwenu. Injili hii inazaa tunda na inaenea ulimwenguni kote. Imekuwa ikifanya hivi ndani yenu pia tangu siku mlipoisikia na kujifunza kuhusu neema ya Mungu katika kweli.Kabla ya mambo yote, eweni na bidii katika upendo kwa kila mmoja, kwa kuwa upendo hautafuti kufunua dhambi za wengine.Kwa sababu hiyo twamshukuru Mungu pia kila wakati. Kwa kuwa wakati mlipo pokea kutoka kwetu ujumbe wa Mungu mliosikia, mlipokea si kama neno la wanadamu. Badala yake, mlipokea kama kweli ilivyo, neno la Mungu. Ni neno hili ambalo linalofanya kazi kati yenu mnaoamini. Kwa hivyo ninyi, ndugu, muwe watu wa kuiga makanisa ya Mungu yaliyoko katika Uyahudi katika Kristo Yesu. Kwa kuwa ninyi pia mliteseka katika mambo yale yale kutoka kwa watu wenu, kama ilivyo kuwa kutoka kwa wayahudi.Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mungu akusaidie wakati wa shida; na jina la Mungu wa Yakobo likulinde na kutuma msaada kutoka mahali patakatifu kwa ajili ya kukutegemeza wewe kutoka Sayuni. Naye akumbuke sadaka yako yote na kuipokea sadaka ya kuteketezwa. Naye akujalie haja za moyo wako na kutimiza mipango yako yote. Ndipo tutakapo shangilia katika ushindi wako, na, katika jina la Mungu wetu, tutapeperusha bendera. Yahwe naakupe maombi yako yote ya haki.Imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu. Maana hivi ndivyo itupasavyo, kwa kuwa imani yenu inakua sana, na upendo wenu kwa kila mtu uongezeke mwingi.Nimesikia upendo na imani uliyonayo katika Bwana Yesu na kwa ajili ya waumini wote. Ninaomba kwamba ushirika wa imani yenu iwe na ufanisi katika ujuzi wa kila jambo jema lililoko kati yetu katika Kristo. Kwa kuwa nimekuwa na furaha na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa sababu mioyo ya waumini imekuwa ikitulizwa nawe, ndugu.Kila mmoja wenu asiangalie tu mahitaji yake binafsi, bali pia ajali mahitaji ya wengine.Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki