Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Mathayo 7:7
Mstari wa Biblia · ULB
Mathayo 7:7
Omba, nawe utapewa. Tafuta, nawe utapata. Bisha hodi, na wewe utafunguliwa.
Katika muktadha
4Unawezaje kusema kwa ndugu yako, ngoja nikutolee kipande kilichomo kwenye jicho lako, wakati kipande cha gogo kimo ndani ya jicho lako?
5Mnafiki wewe; kwanza toa gogo lililomo kwenye jicho lako, na ndipo utakapoweza kuona vizuri na kukitoa kipande cha mti kilichomo kwenye jicho la ndugu yako.
6Usiwape mbwa kilicho kitakatifu, na usiwarushie nguruwe lulu mbele yao. Vinginevyo wataviharibu na kuvikanyaga kwa miguu, na tena watakugeukia wewe na kukurarua vipande vipande.
7Omba, nawe utapewa. Tafuta, nawe utapata. Bisha hodi, na wewe utafunguliwa.
8Kwa yeyote anayeomba, hupokea. Na kwa yeyote anayetafuta, hupata. Na kwa mtu ambaye anayebisha hodi, atafunguliwa.
9Au kuna mtu miongoni mwenu ambaye, ikiwa mtoto wake amemwomba kipande cha mkate atampa jiwe?
10Au ikiwa atamwomba samaki, na yeye atampa nyoka?
Kwa Kiingereza
Ask, and it will be given to you; seek, and you will find; knock, and the door will be opened to you.Marejeo mtambuka
Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.
Chochote mtakachoomba kwa sala, huku mkiamini, mtapokea.”Na chochote tuombacho tutakipokea kutoka kwake, kwa sababu tunazishika amri zake na tunafanya mambo yanayopendeza mbele zake.Ikiwa mtadumu ndani yangu, na kama maneno yangu yakidumu ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtafanyiwa.Kwa hiyo ninawaambia: kila kitu muombacho na kuuliza kwa ajili yake, aminini kwamba mmepokea, navyo vitakuwa vyenu.Yahwe yu karibu na wote wamwitao, wale wamwitao yeye katika uaminifu. Hutimiza haja za wale wanao mheshimu yeye; husikia kilio chao na kuwaokoa.'Niite, na nitakuitika, nitakuelezea mambo makuu, siri ambazo huzielewi.'Lakini kwanza tafuteni ufalme wake na haki yake na haya yote yatakabidhiwa kwako.Kisha mtaniita, na kwenda na kuniomba mimi, na nitawasikiliza. Kwa maana mtanitafuta na kunipata, kwa kuwa mtanitafuta kwa moyo wenu wote.Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki