Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Waefeso 5:11

Mstari wa Biblia · ULB

Waefeso 5:11

Usiwepo ushiriki katika kazi za giza zisizo na matunda, badala yake ziweke wazi.

Soma sura nzima: Waefeso 5

Katika muktadha

8Kwa kuwa ninyi mwanzo mlikuwa giza, lakini sasa mmekuwa nuru katika Bwana. Hivyo tembeeni kama watoto wa nuru.

9Kwa kuwa matunda ya nuru yanajumuisha uzuri wote, haki na ukweli.

10Tafuta kile kinacho furahisha kwa Bwana.

11Usiwepo ushiriki katika kazi za giza zisizo na matunda, badala yake ziweke wazi.

12Kwa sababu mambo yanayofanywa na wao sirini ni aibu sana hata kuyaelezea.

13Mambo yote, yanapofichuliwa na nuru, huwa wazi,

14kwa kuwa Kila kitu kilichofichuliwa kinakuwa nuruni. Hivyo husema hivi, “Amka, wewe uliyelala, na inuka kutoka wafu na Kristo atang'aa juu yako.”

Waefeso 5

Kwa Kiingereza

Berean Standard BibleEphesians 5:11Have no fellowship with the fruitless deeds of darkness, but rather expose them.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Rum 13:12Usiku umeendelea, na mchana umekaribia. Na tuweke pembeni matendo ya giza, na tuvae silaha za nuru.
1 Tim 5:20Waonye wakosaji mbele ya watu wote ili wengine waliobaki labda wataogopa.
2 The 3:6Sasa tunawaagiza, ndugu, katika jina la Bwana Yesu Kristo, kwamba mwepuke kila ndugu ambaye anaishi maisha ya uvivu na siyo kwa kutokana na desturi ambazo mlipokea kutoka kwetu.
2 Yoh 1:10–11Kama mtu anakuja kwenu na haleti fundisho hili, msimkaribishe katika nyumba zenu na msimsalimie. Kwa kuwa amsalimuye hushiriki katika matendo yake maovu.
Rum 16:17Sasa nawasihi, ndugu, kutafakari juu ya hao ambao wanasababisha mgawanyiko na vipingamizi. Wanakwenda kinyume na mafundisho ambayo mmekwisha kujifunza. Geukeni mtoke kwao.
2 The 3:14Ikiwa mtu yeyote hataki kutii neno letu katika waraka huu, mwe makini naye na msiwe na ushirika pamoja naye, ili kwamba aweze kuaibika.
Zab 1:1–2Amebarikiwa mtu yule asiye enenda katika ushauri wa waovu, au kusimama katika njia ya wenye dhambi, au kukaa katika kusanyiko la wenye mizaha. Bali yeye huifurahia sheria ya Yahwe, na huitafakari sheria yake mchana na usiku.
Ufu 18:4Kisha nilisikia sauti nyingine kutoka mbinguni iikisema, “Tokeni kwake watu wangu, ili msije mkashiriki katika dhambi zake, na ili msije mkapokea mapigo yake yoyote.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki