Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 26 Septemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 13 Septemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 26 Septemba 2027
Jumapili · Sauti ya 5
Sikukuu na watakatifu
Jumapili ya 14 baada ya Pentekoste
Jumapili kabla ya Kutukuzwa kwa Msalaba
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Sala ya Jioni: somo
22Sulemani alisimama mbele ya madhabahu ya BWANA, mbela ya mkusanyiko wote wa Waisraeli, naye akanyosha mikono yake kuelekea mbinguni. 23Akasema, “BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe juu mbinguni au chini duniani, ambaye hutunza agano lake kwa uaminifu kwa watumishi wako ambao hutembea mbele yako kwa mioyo yao yote; 27Je, ni kweli kwamba Mungu ataishi duniani? Tazama, Ulimwengu wote na mbingu hazikutoshi - sembuse nyumba hii niliyoijenga! 28Kwa hiyo Mungu naomba uyajali maombi haya ya mtumishi wako na maombi yake, BWANA, Mungu wangu; sikiliza kilio na maombi ambayo mtumishi wako anakuomba leo. 29Naomba ulitazame hekalu hili mchana na usiku, mahali ambapo ulisema, 'Jina langu na uwepo wangu utakuwa' - ili niweze kuwa nasikiliza maombi ambayo mtumishi wako ataomba mahali hapa. 30Kwa hiyo sikia maombi ya mtumishi wako na ya watu wako Israeli tunapokuwa tunaomba mahali hapa. Ndiyo, sikia kutokea mahali ambapo unaishi, kutoka katika mbingu za mbingu; na unaposikia tafadhali samehe.
Sala ya Jioni: somo
19Kwa hekima Yehova aliweka msingi wa dunia, kwa ufahamu aliziimarisha mbingu. 20Kwa maarifa yake vina vilipasuka na mawingu kudondosha umande wake. 21Mwanangu, zingatia hukumu ya kweli na ufahamu, na wala usiache kuvitazama. 22Vitakuwa uzima wa nafsi yako na urembo wa hisani wa kuvaa shingoni mwako. 23Ndipo utatembea katika njia yako kwa usalama na mguu wako hautajikwaa; 24ulalapo hutaogopa; utakapolala, usingizi wako utakuwa mtamu. 25Usitishwe na hofu ya ghafula au uharibifu uliosababishwa na waovu unapotokea, 26kwa maana Yehova utakuwa upande wako na ataulinda mguu wako usinaswe kwenye mtego. 27Usizuie mema kwa wale wanaoyastahili, wakati utendaji upo ndani ya mamlaka yako. 28Jirani yako usimwambie, “Nenda, na uje tena, na kesho nitakupa,” wakati pesa unazo. 29Usiweke mpango wa kumdhuru jirani yako- anayeishi jirani nawe na yeye anakuamini. 30Usishindane na mtu pasipo sababu, ikiwa hajafanya chochote kukudhuru. 31Usimhusudu mtu jeuri au kuchagua njia zake zozote. 32Maana mtu mjanja ni chukizo kwa Yehova, bali humleta mtu mwaminifu kwenye tumaini lake. 33Laana ya Yehova ipo katika nyumba ya watu waovu, bali huibariki maskani ya watu wenye haki. 34Yeye huwadhihaki wenye dhihaka, bali huwapa hisani watu wanyenyekevu.
Sala ya Jioni: somo
1Hekima amejenga nyumba yake; amechonga nguzo saba kutoka katika miamba. 2Ameandaa wanyama wake kwa chakula cha usiku; ameichanganya divai yake; na kuandaa meza yake. 3Amewatuma watumishi wake kupeleka mialiko na kutoka mahali pa juu sana kwenye mji anaita: 4“Wale wasiofunzwa waje hapa!” anawaambia wale wasionaufahamu. 5Njoo, ule chakula, na unywe divai nimeshaichanganya. 6Acheni njia zenu za kijinga, na mkaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu. 7Yeyote amrekebishaye mwenye dhihaka hukaribisha matusi na yeyote anayemshutumu mtu mbaya atapata madhara. 8Usimshutumu mwenye dhihaka, ama atakuchukia; mshutumu mtu mwenye busara, naye atakupenda. 9Mpe mafundisho mtu mwenye busara, naye atakuwa na busara zaidi; mfundishe mtu mwenye haki, naye ataongeza elimu. 10Hofu ya Mungu ni chanzo cha hekima na maarifa ya Mtakatifu ni ufahamu. 11Maana kwa njia yangu siku zako zitazidishwa na uzima wako utaongezewa miaka.
Injili ya 3 ya Sala ya Alfajiri
9Mapema katika siku ya kwanza ya juma, baada ya kufufuka, alimtokea kwanza Mariamu Magdalena, ambaye kutoka kwake alimtoa mapepo saba. 10Aliondoka na kuwaambia wale ambao walikuwa pamoja naye, wakati walipokuwa wakihuzunika na kutoa machozi. 11Walisikia kwamba ni mzima na ameonekana naye, lakini hawakumwamini. 12Baada ya hayo, akajitokeza katika namna tofauti kwa watu wengine wawili, wakati walipokuwa wakitembea kutoka katika nchi. 13Walienda na kuwaambia wanafunzi wengine waliobaki, lakini hawakuwaamini. 14Yesu baadaye akajitokeza kwa wale kumi na mmoja walipokuwa wameegama katika meza, na akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo, kwa sababu hawakuwaamini wale waliomwona baada ya kufufuka kutoka kwa wafu. 15Akawaambia, “ Enendeni ulimwenguni mwote, na kuhubiri injili kwa viumbe vyote. 16Yeyote aaminiye na kubatizwa ataokolewa, na yule asiyeamini atahukumiwa. 17Ishara hizi zitaambatana na wote waaminio. Kwa jina langu watatoa pepo. Watasema kwa lugha mpya. 18Watashika nyoka kwa mikono yao, na hata wakinywa kitu chochote cha kufisha hakitawadhuru. Wataweka mikono kwa wagonjwa, nao watakuwa wazima”. 19Baada ya Bwana kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 20Wanafunzi wakaondoka na kuhubiri kila mahali, wakati Bwana akifanya kazi nao na kulithibitisha neno kwa miujiza na ishara zikifuatana nao.
Waraka (Jumapili kabla ya Kutukuzwa kwa Msalaba)
11Angalieni ukubwa wa barua nilizowaandikia kwa mkono wangu mwenyewe. 12Wale wanaotaka kufanya mema kwa mtazamo wa mwili ndiyo wenye kuwalazimisha mtahiriwe. Wanafanya hivyo kwa sababu wasiingie kwenye mateso ya msalaba wa Kristo. 13Maana hata hao waliotahiriwa wenyewe hawaishiki sheria. Badala yake wanataka ninyi mtahiriwe ili waweze kujivunia miili yenu. 14Isitokee nikajivuna isipokuwa kwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Ni katika yeye ulimwengu umesulubiwa kwangu na mimi katika ulimwengu. 15Kwa kuwa haijalishi kutahiriwa au kutokutahiriwa kuwa ni kitu. Badala yake uzao mpya ni muhimu. 16Kwa wote wenye kuishi kwa kanuni hii, wawe na amani na rehema iwe juu yao wote, na juu ya Israel ya Mungu. 17Tangu sasa mtu yeyote asinitaabishe, maana nimebeba chapa za Yesu mwilini mwangu. 18Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe na roho zenu, ndugu. Amina.
Waraka
21Sasa ni Mungu ambaye hututhibitisha sisi pamoja nanyi katika Kristo, na alitutuma sisi. 22Aliweka muhuri juu yetu na alitupa Roho katika mioyo yetu kama dhamana ya kile ambacho angetupatia baadaye. 23Badala yake, namsihi Mungu kunishuhudia mimi kwamba sababu iliyonifanya nisije Korintho ni kwamba nisiwalemee ninyi. 24Hii sio kwa sababu tunajaribu kudhibiti jinsi imani yenu inavyotakiwa kuwa. Badala yake, tunafanya pamoja nanyi kwa ajili ya furaha yenu, kama mnavyosimama katika imani yenu. 2:1Kwa hiyo niliamua kwa sehemu yangu mwenyewe kwamba nisingekuja tena kwenu katika hali ya uchungu. 2Kama niliwasababishia ninyi maumivu, ni nani angenifurahisha mimi, lakini ni yule ambaye aliumizwa na mimi? 3Niliandika kama nilivyofanya ili kwamba wakati nikija kwenu nisiweze kuumizwa na wale ambao wangekuwa wamenifanya nifurahi. Ninao ujasiri kuhusu ninyi nyote kwamba furaha yangu ni furaha ile ile mliyonayo ninyi nyote. 4Kwa kuwa niliwaandikia ninyi kutokana na mateso makubwa, na dhiki ya moyo, na kwa machozi mengi. Sikutaka kuwasababishia ninyi maumivu. Badala yake, nilitaka mjue upendo wa kina nilionao kwa ajili yenu.
Waraka (Kanisa la Kaburi Takatifu)
1Kwa hiyo, ndugu watakatifu, washiriki wa wito wa mbinguni, mumfikiri Yesu, Mtume na Kuhani Mkuu wa ukiri wetu. 2Alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemteua, kama Musa alivyokuwa mwaminifu pia katika nyumba yote ya Mungu. 3Kwa kuwa Yesu amehesabiwa kuwa na heshima kubwa kuliko aliyokuwa nayo Musa, kwa sababu yule anayejenga nyumba anahesabiwa kuwa na heshima kubwa kuliko nyumba yenyewe. 4Kwa kuwa kila nyumba hujengwa na mtu fulani, lakini yule anayejenga kila kitu ni Mungu.
Injili (Jumapili kabla ya Kutukuzwa kwa Msalaba)
13Maana hakuna aliyepanda juu kutoka mbinguni isipokuwa yeye aliyeshuka, Mwana wa Adamu. 14Kama vile Musa alivyomwinua nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu lazima ainuliwe, 15ili kwamba wote watakaomwamini wapate uzima wa milele. 16Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, kwamba akamtoa mwanae wa pekee, ili kwamba mtu yeyote amwaminiye asiangamie bali awe na uzima wa milele. 17Kwa sababu Mungu hakumtuma mwanae duniani ili auhukumu ulimwengu, bali kwamba ulimwengu uokolewe katika yeye.
Injili
1Yesu alisema nao tena katika mifano, akisema, 2“Ufalme wa mbinguni unafanana na mfalme aliyeandaa sherehe ya harusi ya mwanawe. 3Akawatuma watumishi wake kuwakaribisha waliokuwa wamealikwa kuja katika sherehe ya harusi, lakini hawakufika. 4Mfalme aliwatuma tena watumishi wengine, akisema. “Waambieni wote walioalikwa, Angalieni, nimeandaa chakula. Fahali na ndama wangu wanono wamechinjwa, na mambo yote yako tayari, Njoni katika sherehe ya harusi.” 5Lakini watu hao hawakuzingatia kwa dhati mwaliko wake. Baadhi walirejea katika mashamba yao, na wengine walirudi katika sehemu zao za biashara. 6Wengine waliwainukia watumishi wa mfalme na kuwadharirisha na kuwaua. 7Lakini mfalme alikasirika. Alituma jeshi lake, akawaua wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto. 8Kisha aliwaambia watumishi wake, “Harusi iko tayari, lakini walioalikwa hawakustahili. 9Kwa hiyo nendeni kwenye makutano ya njia kuu, waalikeni watu wengi kadri iwezekanavyo waje kwenye sherehe ya harusi.” 10Watumishi walienda njia kuu na kuwakaribisha watu wowote waliowaona, wema na wabaya. Hivyo ukumbi wa harusi ulijaa wageni. 11Lakini mfalme alipoingia kuwatazama wageni, alimuona mtu mmoja ambaye hakuvaa vazi rasmi la harusi! 12Mfalme alimwuliza, 'Rafiki, ulipataje kufika hapa ndani bila vazi la harusi?' Na mtu huyo hakujibu chochote. 13Ndipo mfalme alipowaambia watumishi wake, “Mfungeni mtu huyu mikono na miguu na mtupeni nje katika giza, huko ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno. 14Kwa kuwa watu wengi wanaitwa, lakini wateule ni wachache.”
Injili (Kanisa la Kaburi Takatifu)
13Wakati Yesu alipofika sehemu za Kaisaria ya Filipi, akawauliza wanafunzi wake, akisema, “Watu wanasema kuwa Mwana wa Mtu ni nani?” 14Wakasema,” Wengine husema kuwa ni Yohana Mbatizaji; wengine, Eliya; na wengine, Yeremia, au mojawapo wa manabii. 15Akawaambia, ninyi mwasema mimi ni nani? 16Kwa akijibu, Simoni Petro akasema, “Wewe ni Kristo Mwana wa Mungu aliye hai” 17Yesu akamjibu na kumwambia, “Umebarikiwa wewe, Simoni Bar Yona, kwa kuwa damu na nyama havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18Nami pia ninakwambia kuwa wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu. Milango ya kuzimu haitalishinda.
Watakatifu wa siku
- Kumbukumbu ya kuwekwa wakfu kwa kanisa la Ufufuo wa Kristo huko Yerusalemu (335)
- Kabla ya Sikukuu ya Kutukuzwa kwa Msalaba wenye Thamani Utoao Uzima wa Bwana
- Mfiadini wa Kikasisi Kornelio, akida (karne ya 1)
- Wafiadini wa Kikasisi Stefano na Aleksanda, mapadri, na Nikolao, shemasi (1937)
- Wafiadini Kronida, Leontio, Seleuko, Stratoniko na Serapioni (karibu 237)
- Wafiadini Makrobio, Gordiano, Eliya, Zotiko, Lukiano na Valeriani (320)
- Mfiadini wa Kikasisi Yuliani, padri (karne ya 4)
- Mtakatifu Mtawa Petro wa Atroa (karne ya 9)
- Mfiadini Mkuu Ketevan, malkia wa Kakheti (1624)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 13 Septemba katika kalenda ya kanisa ni 26 Septemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki