Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 25 Septemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 12 Septemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 25 Septemba 2027
Jumamosi · Wiki ya 14 baada ya Pentekoste · Sauti ya 4
Sikukuu na watakatifu
Jumamosi kabla ya Kutukuzwa kwa Msalaba
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka (Jumamosi kabla ya Kutukuzwa kwa Msalaba)
6Sasa tunaizungumza hekima miongoni mwa watu wazima, lakini si hekima ya dunia hii, au ya watawala wa nyakati hizi, ambao wanaopita. 7Badala yake, tunaizungumza hekima ya Mungu katika ukweli uliofichika, hekima iliyofichika ambayo Mungu aliichagua kabla ya nyakati za utukufu wetu. 8Hakuna yeyote wa watawala wa nyakati hizi aliyeijua hekima hii, Kama wangeifahamu katika nyakati zile, wasingelimsulubisha Bwana wa utukufu. 9Lakini kama ilivyoandikwa, “Mambo mbayo hakuna jicho limeyaona, hakuna sikio lililoyasikia, mawazo hayakufikiri, mambo ambayo Mungu ameyaandaa kwa ajili ya wale wampendao yeye.”
Waraka
1Hivi ndivyo mtu atuhesabu sisi, kama watumishi wa Kristo na mawakili wa siri za kweli za Mungu. 2Katika hili, kinachotakiwa kwa uwakili ni kwamba wawe wa kutumainiwa. 3Lakini kwangu mimi ni kitu kidogo sana kuwa ninahukumiwa na ninyi au hukumu ya kibinadamu. Kwa kuwa sijihukumu hata mimi mwenyewe. 4Sijihukumu mimi mwenyewe, hii haina maana kuwa mimi ni mwenye haki. Ni Bwana anihukumuye. 5Kwa hiyo, msitamke hukumu juu ya lolote kabla ya wakati, kabla ya kuja kwa Bwana. Atayaleta nuruni mambo yaliyofichika gizani na kufunua makusudi ya mioyo. Ndipo kila mmoja atapokea sifa yake kutoka kwa Mungu.
Waraka (Mama wa Mungu)
5Muwe na nia kama aliyonayo Kristo Yesu. 6Ingawaje yeye ni sawa na Mungu. Lakini hakujali kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho. 7Badala yake, alijishusha mwenyewe. Alichukua umbo la mtumishi. Akajitokeza katika mfano wa wanadamu. Alionekana mwanadamu. 8Yeye alijinyeyekeza na kuwa mtii hadi kifo, kifo cha msalaba. 9Hivyo basi Mungu alimtukuza sana. Alimpa jina kuu lipitalo kila jina. 10Alifanya hivyo ili kwamba katika jina la Yesu kila goti sharti liiname. Magoti ya walio mbinguni na walio juu ya ardhi na chini ya ardhi. 11Na alifanya hivyo ili kwamba kila ulimi sharti ukiri kwamba Yesu kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
Injili (Jumamosi kabla ya Kutukuzwa kwa Msalaba)
37Yeye ambaye anampenda baba au mama zaidi kuliko mimi huyo hanistahili. Na yeye anayempenda kijana au binti zaidi kuliko mimi huyo hanistahili. 38Yeye ambaye hatabeba msalaba na kunifuata mimi hanistahili. 39Yeye atakayetafuta maisha atayapoteza. Lakini yeye atakayepoteza maisha kwa ajili yangu atayapata. 40Yeye atakayewakaribisha amenikaribisha mimi, na yeye atakayenikaribisha mimi amemkaribisha yeye aliyenituma mimi. 41Na yeye atakayemkaribisha nabii kwa sababu ni nabii atapokea thawabu ya nabii. Na yeye atakayemkaribisha mwenye haki kwa sababu ni mtu wa haki atapokea thawabu ya mtu wa haki. 42Yeyote atakayempatia mmoja wa wadogo hawa, hata kikombe cha maji ya kunywa ya baridi, kwa sababu yeye ni mwanafunzi, kweli ninawaambia, yeye hawezi kukosa kwa njia yeyote thawabu yake.” 11:1Ikawa baada ya Yesu kumaliza kuwaelekeza wanafunzi wake kumi na wawili aliondoka plae kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao,
Injili
1Baadaye aliongea na umati wa watu na wanafunzi wake. Akasema, 2“Waandishi na Mafarisayo wanakalia kiti cha Musa. 3Kwa hiyo chochote wanacho waamuru kufanya, fanyeni huku mkiwachunguza. Lakini msije mkaiga matendo yao, kwa sababu wao hutamka mambo wasiyoyafanya. 4Kweli, wao hufunga mizigo mizito ambayo ni vigumu kuibeba, na kisha huwabebesha watu mabegani mwao. Lakini wao wenyewe hawasogezi hata kidole kuibeba. 5Matendo yao yote, huyafanya ili watazamwe na watu. Kwa sababu wao hupanua masanduku yao na huongeza ukubwa wa mapindo ya mavazi yao. 6Wao hupendelea kukaa maeneo ya kifahari katika sherehe na katika viti vya heshima ndani ya masinagogi, 7na kusalimiwa kwa heshima maeneo ya sokoni, na kuitwa “Walimu” na watu. 8Lakini ninyi hampaswi kuitwa “Walimu,” Kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja, na ninyi wote ni ndugu. 9Msimuite mtu yeyote hapa duniani kuwa baba yenu, kwa kuwa mnaye Baba mmoja tu, naye yuko mbinguni. 10Wala msije kuitwa 'walimu,' kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja tu, yaani Kristo. 11Bali aliye mkubwa miongoni mwenu atakuwa mtumishi wenu. 12Yeyote ajiinuae atashushwa. Na yeyote anaye jishusha atainuliwa.
Injili (Mama wa Mungu)
38Sasa walipokuwa wakisafiri, waliingia katika kijiji fulani, na mwanamke mmoja jina lake Martha alimkaribisha nyumbani kwake. 39Alikuwa na dada aliyeitwa Mariamu, aliekaa miguuni pa Bwana na kusikiliza neno lake. 40Lakini Martha alijipa shughuli nyingi za kuandaa mlo. Alikwenda kwa Yesu, na kusema, “Bwana, haujali kwamba dada yangu ameniacha nihudumu peke yangu? Hivyo basi mwambie anisaidie.” 41Lakini Bwana alimjibu na kumwambia, “Martha, Martha, una sumbuka juu ya mambo mengi, 42lakini ni kitu kimoja tu cha muhimu. Mariamu amechagua kilicho chema, ambacho hakitaondolewa kutoka kwake.” 11:27Ilitokea kwamba alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke fulani alipasa sauti yake zaidi ya wote kwanye mkutano wa watu na kusema “ Limebarikiwa tumbo lililo kuzaa na matiti uliyoyanyonya” 28Lakini yeye akasema, wamebarikiwa wale wasikio neno la Mungu na kulitunza.
Watakatifu wa siku
- Kufungwa kwa Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Mama Mtakatifu Sana wa Mungu
- Mfiadini wa Kikasisi Autonomo, askofu wa Italia (313) [ibada huimbwa tarehe 11]
- Mtakatifu Mtawa Athanasio wa Vysotsk, mtenda miujiza wa Serpukhov (1395)
- Wafiadini wa Kikasisi Theodoro, Yohana, Nikolao, mapadri, na Mfiadini Aleksi (1937)
- Mfiadini wa Kikasisi Kornuto, Askofu wa Nikomedia (wa Ikonio) (karibu 249-259)
- Mfiadini Yuliani na pamoja naye wafiadini 40 (karne ya 4)
- Mtakatifu Mtawa Basiani wa Tiksna (1624)
- Kuhamishwa kwa masalia ya Mwenye Haki Simeoni wa Verkhoturye (1704)
- Mfiadini wa Kikasisi Theodoro, Askofu wa Aleksandria
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 12 Septemba katika kalenda ya kanisa ni 25 Septemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki