Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Mafundisho

Injili kando kwa kando · Mafundisho

Mfano wa mpanzi

Mt 13:1–9 · Mk 4:1–9 · Lk 8:4–8

Mathayo

Mt 13:1–9

1Katika siku hiyo Yesu aliondoka nyumbani na kukaa kando ya bahari.

2Umati mkubwa ulikusanyika kwa kumzunguka, aliingia ndani ya mtumbwi na kukaa ndani yake. Umati wote walisimama kando ya bahari.

3Kisha Yesu alisema maneno mengi kwa mifano, Alisema, “Tazama, mpanzi alienda kupanda.

4Alipokuwa akipanda baadhi ya mbegu zilianguka kando ya njia na ndege walikuja wakazidonoa.

5Mbegu zingine zilianguka juu ya mwamba, ambapo hazikupata udongo wa kutosha. Ghafla zilichipuka kwa sababu udongo haukuwa na kina.

6Lakini jua lilipo chomoza zilichomwa kwa sababu hazikuwa na mizizi, na zilikauka.

7Mbengu zingine zilianguka kati ya miti yenye miiba. Miti yenye miiba ilirefuka juu ikaisonga.

8Mbegu zingine zilianguka kwenye udongo mzuri na kuzaa mbegu, zingine mara mia moja zaidi, zingine sitini na zingine thelathini

9Aliye na masikio na asikie.

Marko

Mk 4:1–9

1Tena alianza kufundisha kandokando ya bahari. Na umati mkubwa ulikusanyika ukamzunguka, akaingia ndani ya mtumbwi baharini, na kukaa. Umati wote walikuwa pembeni mwa bahari ufukweni.

2Na akawafundisha mambo mengi kwa mifano, na akasema kwao kwa mafundisho yake.

3Sikilizeni, mpanzi alienda kupanda.

4Alipokuwa akipanda, baadhi ya mbegu zilianguka njiani, na ndege wakaja wakazila.

5Mbegu zingine zilianguka kwenye mwamba, ambako hapakuwa na udongo mwingi. Mara zikanyauka, kwa sababu hazikuwa na udongo wakutosha.

6Lakini jua lilipochomoza, zilinyauka, na kwa sababu hazikuwa na mzizi, zilikauka.

7Mbegu ziingine zilianguka katikati ya miiba. Miiba ilikua na ikazisonga, na hazikuzaa matunda yeyote.

8Mbegu zingine zilianguka kwenye udongo mzuri na zikazaa matunda wakati zikikua na kuongezeka, zingine zilizaa mara thelathini zaidi, na zingine sitini, na zingine mia”.

9Na akasema, “Yeyote mwenye masikio ya kusikia, na asikie!”

Luka

Lk 8:4–8

4Nabaada ya umati wa watu kukusanyika pamoja, wakiwemo na watu waliokuja kwake kutoka miji mbalimbali, akazungumza nao kwa kutumia mifano.

5“mpandaji alienda kupanda mbegu, alipokuwa apanda, baadhi ya mbegu hizo ziliangukia kando ya njia zikakanyagwa chini ya miguu, na ndege wa angani wakazila.

6Mbegu zingine zilianguka juu ya udongo wa miamba na zilipoota na kuwa miche zilipooza kwa sababu hakukuwa na unyevunyevu.

7Mbegu zingine ziliangukia kwenye miti ya miiba, nayo hiyo miti ya miiba ikakua pamoja na zile mbegu na zikasongwa.

8Lakini mbegu zingine ziliangukia kwenye udongo unaofaa na zikazaa mazao mara mia zaidi. “Baada ya Yesu kusema mambo haya, alipaza sauti,”Yeyote aliye na masikio ya kusikia na asikie.”

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY