Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Mafundisho

Injili kando kwa kando · Mafundisho

Kumkufuru Roho

Mt 12:31–32 · Mk 3:28–30 · Lk 12:10

Mathayo

Mt 12:31–32

31Kwa hiyo nasema kwenu, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, ila kumkufuru Roho Mtakatifu hawatasamehewa.

32Na yeyote asemaye neno kinyume cha Mwana wa Adamu, hilo atasamehewa. Lakini yeyote asemaye kinyume na Roho Mtakatifu, huyo hatasamehewa, katika ulimwengu huu, na wala ule ujao

Marko

Mk 3:28–30

28Kweli nawambieni, dhambi zote za wana wa watu zitasamehewa, pamoja na kufuru ambazo wanatamka,

29lakini yeyote atakaye mkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, bali ana hatia ya dhambi ya milele”.

30Yesu alilisema hili kwa sababu walikuwa wakisema, “Ana roho chafu”.

Luka

Lk 12:10

10Yeyote atakayesema neno baya juu ya Mwana wa Adamu, atasamehewa, lakini yeyote atakayemkufuru Roho Mtakatifu, hatasamehewa.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY