Gundua › Injili kando kwa kando › Katika Galilaya
Injili kando kwa kando · Katika Galilaya
Yesu aenda kuhubiri katika miji mingine
Mk 1:35–39 · Lk 4:42–44
Mk 1:35–3935Aliamka asubuhi na mapema, wakati ilikuwa bado giza; aliondoka na kwenda mahali pa faragha na aliomba huko.
36Simoni na wote waliokuwa pamoja naye walimtafuta.
37Walimpata na wakamwambia, “Kila mmoja anakutafuta”
38Aliwaambia, “Twendeni mahali pengine, nje katika miji inayozunguka, ili niweze kuhubiri huko pia. Ndiyo sababu nilikuja hapa.”
39Alikwenda akipita Galilaya yote, akihubiri katika masinagogi yao na kukemea pepo.
Lk 4:42–4442Wakati kulipopambazuka, alienda eneo lisilokuwa na watu. Makutano ya watu walikuwa wakimtafuta na wakaja katika eneo alilokuwapo. Walijaribu kumzuia asiende mbali na wao.
43Lakini akawaambia, “Lazima pia nihubiri habari njema za ufalme wa Mungu katika miji mingine mingi, kwa kuwa hii ndiyo sababu nilitumwa hapa.”
44Kisha aliendelea kuhubiri ndani ya masinagogi katika uyahudi wote.
Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.
Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY