1Wakati Yesu aliposhuka chini kutoka mlimani, umati mkubwa ulimfuata.
2Tazama, mkoma alikuja na kusujudu mbele yake, akasema, “Bwana, ikiwa uko tayari, unaweza kunifanya niwe safi”.
3Yesu akanyoosha mkono wake na kumgusa, akasema, “Niko tayari. Uwe msafi.” Hapo hapo alitakaswa ukoma wake.
4Yesu akamwambia, “Angalia kwamba usiseme kwa mtu yeyote. Shika njia yako, na jioneshe mwenyewe kwa kuhani na utoe zawadi ambayo Musa aliagiza, kwa ajili ya ushuhuda kwao”