Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Mateso

Injili kando kwa kando · Mateso

Yuda akubali kumsaliti Yesu

Mt 26:14–16 · Mk 14:10–11 · Lk 22:3–6

Mathayo

Mt 26:14–16

14Ndipo mmoja wa wale Kumi na wawili, aliyeitwa Yuda Iskariote, alienda kwa wakuu wa makuhani

15na kusema, “Mtanipatia nini nikimsaliti?” Wakampimia Yuda vipande thelathini vya fedha.

16Tangu muda huo alitafuta nafasi ya kumsaliti.

Marko

Mk 14:10–11

10Kisha Yuda Iskariote, mmoja wa wale kumi na wawili, alikwenda kwa wakuu wa makuhani ili kwamba apate kumkabidhi kwao.

11Wakati wakuu wa Makuhani waliposikia hivyo, walifurahi na wakaahidi kumpa fedha. Alianza kutafuta nafasi ya kumkabidhi kwao.

Luka

Lk 22:3–6

3Shetani akaingia ndani ya Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi Kumi na mbili.

4Yuda akaenda kujadiliana na wakuu wa makuhani na wakuu namna ambavyo atamkabidhi Yesu kwao.

5Walifurahi, na kukubaliana kumpa fedha.

6Yeye aliridhia, na alitafuta fursa ya kumkabidhi Yesu kwao mbali na kundi la watu.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY