Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Mateso

Injili kando kwa kando · Mateso

Yesu apakwa mafuta Bethania

Mt 26:6–13 · Mk 14:3–9 · Yn 12:1–8

Mathayo

Mt 26:6–13

6Wakati Yesu alipokuwa Bethania katika nyumba ya Simoni mkoma,

7alipokuwa amejinyoosha mezani, mwanamke mmoja alikuja kwake akiwa amebeba mkebe wa alabasta iliyokuwa na mafuta yenye thamani kubwa, na aliyamimina juu ya kichwa chake.

8Lakini wanafunzi wake walipoona jambo hilo, walichukia na kusema, “Nini sababu ya hasara hii?

9Haya yangeweza kuuzwa kwa kiasi kikubwa na kupewa maskini.”

10Lakini Yesu, akiwa anajua hili, aliwaambia, “Kwa nini mnamsumbua mwanamke huyu? Kwa kuwa amefanya kitu kizuri kwangu.

11Masikini mnao siku zote, lakini hamtakuwa pamoja nami daima.

12Kwa sababu alipomimina mafuta haya juu ya mwili wangu, alifanya hivyo kwa ajili ya maziko yangu.

13Kweli nawaambieni, popote Injili hii itakapohubiriwa katika ulimwengu mzima, kitendo alichofanya huyu mwanamke, pia kitakuwa kinasemwa kwa ajili ya kumkumbuka.”

Marko

Mk 14:3–9

3Wakati Yesu alipokuwa Bethania nyumbani kwa Simoni mkoma, na alipokuwa akielekea mezani, mwanamke mmoja alikuja kwake akiwa na chupa ya marashi ya nardo safi yenye gharama kubwa sana, aliivunja chupa na kuimimina juu ya kichwa chake.

4Lakini kulikuwa na baadhi yao waliokasirika. Waliambiana wao kwa wao wakisema, “Ni nini sababu ya upotevu huu?

5Manukato haya yangeweza kuuzwa kwa zaidi ya dinari mia tatu, na wakapewa maskini.” Nao walimkemea.

6Lakini Yesu alisema, “Mwacheni peke yake. Kwa nini mnamsumbua? Amefanya jambo zuri kwangu.

7Siku zote maskini mnao, na wakati wowote mnapotamani mnaweza kufanya mazuri kwao, lakini hamtakuwa nami wakati wote.

8Amefanya kile anachoweza: ameupaka mwili wangu mafuta kwa ajili ya maziko.

9Kweli nawaambia, kila mahali injili inapohubiriwa katika ulimwengu wote, kile alichofanya mwanamke huyu kitazungumzwa kwa ukumbusho wake.

Yohana

Yn 12:1–8

1Siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alienda Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye alimfufua kutoka katika wafu.

2Basi wakamwandalia chakula cha jioni huko, na Martha akamtumikia, wakati huo Lazaro alikuwa mmoja wapo wa wale walioketi chakulani pamoja na Yesu.

3Kisha Mariamu akachukua ratli ya manukato yaliyotengenezwa kwa nardo safi, yenye thamani kubwa, akampaka Yesu miguuni, na kumfuta miguu kwa nywele zake; nyumba yote ilijaa harufu ya manukato.

4Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi wake, ambaye ndiye atakayemsaliti Yesu, akasema,

5“Kwanini manukato haya yasingeuzwa kwa dinari mia tatu na wakapewa maskini?”

6Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini, bali kwa sababu alikuwa mwizi: yeye ndiye aliyeshika mfuko wa fedha na alikuwa anachukua baadhi ya vilivyowekwa humo kwa ajili yake mwenyewe.

7Yesu alisema, “Mwache aweke alicho nacho kwa ajili ya siku ya maziko yangu.

8Maskini mtakuwa nao siku zote; lakini hamtakuwa nami siku zote.”

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY