Gundua › Injili kando kwa kando › Njiani kwenda Yerusalemu
Injili kando kwa kando · Njiani kwenda Yerusalemu
Nani aliye mkuu zaidi
Mt 18:1–5 · Mk 9:33–37 · Lk 9:46–48
Mt 18:1–51Muda huo huo wanafunzi wakaja kwa Yesu na kumwambia, “Ni nani aliye mkubwa katika ufalme wa mbinguni?”
2Yesu akamwita mtoto mdogo, akamweka katikati yao,
3na kusema, “Kweli nawaambieni, msipotubu na kuwa kama watoto wadogo hamtaweza kuingia katika ufalme wa Mungu.
4Hivyo yeyote ajishushaye kama mtoto mdogo, mtu kama huyo ni mkuu katika ufalme wa mbinguni.
5Na yeyote ampokeaye mtoto mdogo kwa jina langu anipokea mimi.
Mk 9:33–3733Ndipo walifika Karperinaumu. Wakati akiwa ndani ya nyumba aliwauliza, ''Mlikuwa mnajadili nini njiani”?
34Lakini walikuwa kimya. Kwani walikuwa wanabishana njiani kwamba nani alikuwa mkubwa zaidi.
35Alikaa chini akawaita kumi na wawili pamoja, na alisema nao, “Kama yeyote anataka kuwa wa kwanza, ni lazima awe wa mwisho na mtumishi wa wote.”
36Alimchukua mtoto mdogo akamweka katikati yao. Akamchukua katika mikono yake, akasema,
37“Yeyote ampokeaye mtoto kama huyu kwa jina langu, pia amenipokea mimi, na ikiwa mtu amenipokea, hanipokei mimi tu, lakini pia aliyenituma.”
Lk 9:46–4846Kisha mgogoro ulianza ulizuka miongoni mwao i juu ya nani angekuwa mkuu.
47Lakini Yesu alipotambua walichokuwa wakihojiana mioyoni mwao, alimchukua mtoto mdogo, na kumuweka upande wake,
48na akasema, “ kama mtu yeyote akimpokea mtoto mdogo kama huyu kwa jina langu, anipokea mimi pia, na yeyote akinipokea mimi, ampokea pia aliyenituma, kwa kuwa aliye mdogo kati yenu wote ndiye alie mkuu”
Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.
Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY