18Asubuhi alipokuwa anarudi mjini, alikuwa na njaa.
19Aliona mtini kandokando ya barabara. Akauendea, lakini hakupata kitu juu yake isipokuwa majani. Aliuambia, “Kusiwe na matunda kwako daima tena.” Na mara hiyo mtini ule ukanyauka.
20Wanafunzi walipoona, wakastaajabu na kusema, “Imekuwaje mtini umenyauka mara moja?”
21Yesu akajibu na kuwaambia, “Kweli nawaambieni, kama mkiwa na imani na bila wasiwasi, hamtafanya kile kilichofanyika kwa huo mtini tu, lakini mtauambia hata huo mlima, ' uchukuliwe na ukatupwe baharini, 'na itafanyika.
22Chochote mtakachoomba kwa sala, huku mkiamini, mtapokea.”