23Yesu alipofika hekaluni, wakuu wa makuhani na wazee wa watu wakamjia wakati alipokuwa akifundisha na kumwuliza, “Ni kwa mamlaka gani unafanya mambo haya? Na ni nani aliyekupa mamlaka haya?”
24Yesu akajibu na kuwaambia, “Nami tena nitawauliza swali moja. kama mkiniambia, nami vilevile nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.
25Ubatizo wa Yohana- ulitoka wapi, mbinguni au kwa wanadamu?” Wakahojiana wenyewe, wakisema, tukisema, ulitoka mbinguni, 'atatuambia, kwa nini hamkumwamini? '
26Lakini tukisema, 'ulitoka kwa wanadamu, 'tunawaogopa makutano, kwa sababu wote wanamwona Yohana kama nabii.”
27Kisha wakamjibu Yesu na kusema, “Hatujui” Akawaambia pia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani nafanya mambo haya.