Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 23 Aprili
Kalenda ya Kiorthodoksi · 10 Aprili (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 23 Aprili 2027
Ijumaa · Wiki ya 6 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 5
Sikukuu na watakatifu
Wafiadini Terenti, Pompio, Afrikano, Maksimo, Zenoni, Aleksanda, Theodoro na wengine 33 (karibu 249-251)
Kwaresima Kuu
Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Saa ya 6
10Furahia na Yerusalemu na fuhahia kwa ajili yake, ninyi nyote mnaopenda yeye; furahia pamoja na yeye, ninyi mnaomboleza juu yake! 11Maana utamuuguza na ataridhika, katika maziwa yake atakufariji; utakunywa mpaka ushibe na kufurahia kwa wingi wa utukufu wake. 12Yahwe asema hivi, ''Ni nanakaribia kutawanya mafanikio juu katika mto, na utajiri wa mataifa kama wingi wa mkondo wa maji. Utamuuguza kwa upande wake, na kubebwa katika mikono yake, mtabebwa juu ya magoti yake. 13Kama vile mama anavyomfariji mtoto wake, hivyo basi nami nitawafariji ninyi, na mtapata faraja katika Yerusalemu.'' 14Utayaona haya, na moyo wako utafurahia, na mifupa yako itachipukia kama zabuni ya nyasi. Aridhi ya Yahweitajulikana kwa watumishi wake, lakini atawaonyesha hasira yake dhidi ya maadui zake. 15Kwa kutazama, Yahwe anakuja kwa moto, na gari lake linakuja kama upepo wa dhoruba kuleta joto katika hasira yake na kukemea kwake ni kama moto uwakao. 16Maana Yahwe ametekeleza hukumu juu ya watu kwa moto na kwa upanga wake. Wale watakaouliwa na Yahwe watakuwa wengi. 17Watajiweka wakfu wenyewe na kujisafisha wenywe, ili waweze kuingia katika bustani, kumfuata aliyeko katikati ya wale walao nyama ya nguruwe na vitu haramu kama panya. ''Watafika mwisho - hili ni tamko la Yahwe. 18Maana ninayajua matendo yao na mawazo yao. Wakatiutafika nitakapoyakusanya mataifa yote na lugha zote. Watakuja na kuona utukufu wangu. 19Nitaweka ishara ya ukuu wangu miongoni mwao. Halafu nitawatuma wakazi kutoka miongoni mwao kwa mataifa. Kwa Tarshishi, Puti, na Ludi, upinde wale wanaochukua upinde wao, kwa Tubali, Javani, na umbali kuelekea katika pwani kule ambapo hawajasikia chochote kuhusu mimi wala kuona utukufu wangu. Watatangaza utukufu wangu miongoni mwa mataifa. 20Watawaleta kaka zako wote nje ya mataifa yote, kama sadaka kwa Yahwe. Watakuja kwa farasi na kwa gari, na kwa gari, juu ya nyumbu na juu ya ngamia, kuelekea mlima wangu mtakatifu Yerusalemu - asema Yahwe. Maana watu wangu wa Israeli wataleta sadaka ya mavuno kwenye vyombo visafi katika nyumba ya Yahwe. 21Baadhi ya vitu hivi nitavichagua kama makuhani na walawi — asema Yahwe. 22Maana itakuwa mbingu mpya na nchi mpya ambayo nitakayoifanya ibaki mbele zangu— Hili ndilo tamko la Yahwe— Hivyo ndivyo ukoo wenu utakavyobakia, na jina lenu litabaki. 23Kutoka mwenzi mmoja mpaka mwingine, na kutoka sabato moja mpaka nyingine, watu wote watakuja kukuinamia chini— asema Yahwe. 24Watakwenda nje na kuona miili ya wafu ya watu walioniasi mimi, maana wadudu wawalao wao hatakufa, na moto huwaunguzao hautazimika; na itakuwa ni chuki kwa wale wote wenye mwili.''
Sala ya Jioni: somo
33Yakobo alipomaliza maagizo hayo kwa wanawe, akaiweka miguu yake kitandani, akakata roho, akawaendea watu wake 50:1Yusufu akahuzunika sana hata akauangukia uso wa baba yake, akamlilia, na kumbusu. 2Yusufu akawaagiza watumishi wake matabibu kumtia dawa babaye. Hivyo matabibu wakampaka dawa Israeli. 3Wakatimiza siku arobain, kwani huo ndio uliokuwa muda kamili wa kutia dawa. Wamisri wakamlilia kwa siku sabini 4Siku za maombolezo zilipotimia, Yusufu akaongea na watumishi wa baraza la kifalme wa Farao kusema, “Ikiwa nimepata kibali machoni penu, tafadharini ongeeni na Farao, kusema, 5'Baba yangu aliniapisha, kusema, “Tazama, ninakaribia kufa. Unizike katika kaburi nililolichimba kwa ajili yangu mwenyewe katika nchi ya Kanaani. Ndipo utakaponizika.” Basi sasa niruhusu niende nimzike baba yangu, na kisha nitarudi.” 6Farao akajibu, “Nenda na umzika baba yako, kama alivyokuwapisha.” 7Yusufu akaenda kumzika baba yake. Maofisa wa Farao wote wakaenda pamoja naye - washauri wa nyumba yake, maofisa waandamizi wote wa nchi ya Misri, 8pamoja na nyumba yote ya Yusufu na ndugu zake, na nyumba yote ya baba yake. Lakini watoto wao, kondoo wao na makundi ya mbuzi wao yaliachwa katika nchi ya Gosheni. 9Vibandawazi na wapanda farasi pia walikwenda pamoja naye. Lilikuwa kundi kubwa sana la watu. 10Hata walipokuja katika sakafu ya kupuria ya Atadi upande mwingine wa Yordani, wakaomboleza kwa majonzi ya huzuni kubwa. Yusufu akafanya maombolezo ya siku saba kwa ajili ya babaye pale. 11Wenyeji wa nchi, Wakanaani, walipoona maombolezo katika sakafu ya Atadi, wakasema, “Hili ni tukio la kuhuzunisha sana kwa Wamisri.” Ndiyo maana eneo hilo likaitwa Abeli Mizraimu, lililoko mbele ya Yordani. 12Hivyo wanawe wakamfanyia Yakobo kama alivyokuwa amewaagiza. 13Wana wake wakampeleka katika nchi ya Kanaani na wakamzika katika pango katika shamba la Makpela, karibu na Mamre. Ibrahimi alikuwa amelinunua pango pamoja na shamba kwa ajili ya eneo la kuzikia. Alikuwa amelinunua kutoka kwa Efroni Mhiti. 14Baada ya kuwa amemzika babaye, Yusufu akarudi Misri, yeye, pamoja na ndugu zake, na wote waliokuwa wamemsindikiza ili kumzika babaye. 15Nduguze Yusufu walipoona kwamba baba yao amekufa, wakasema, “Itakuwaje ikiwa Yusufu atatukasirikia na akataka kutulipa kikamilifu kwa ajili ya uovu tuliomtenda?” 16Hivyo wakamwagiza Yusufu, kusema, “Baba yako alitoa maelekezo kabla hajafa, kusema, 17'Mwambieni hivi Yusufu, “Tafadhari samehe makosa ya ndugu zako na dhambi yao uovu waliokutenda.” Basi wasamehe watumishi wa Mungu wa baba yako.” Yusufu akalia walipomwambia. 18Ndugu zake pia wakaenda na kuinamisha nyuso zao mbele zake. Wakasema, “Tazama, sisi ni watumishi wako.” 19Lakini Yusufu akawajibu, “Msiogope, Je mimi ni badala ya Mungu? 20Lakini kwenu, mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema, kuhifadhi maisha ya watu wengi, kama mwonavyo leo. 21Hivyo basi msiogope. Nitawahudumia ninyi na watoto wenu wadogo.” Kwa njia hii aliwatia moyo na kuongea na mioyo yao kwa upole. 22Yusufu akakaa Misri, pamoja na familia ya baba yake. Akaishi miaka mia moja na kumi. 23Yusufu akawaona wana wa Efraimu hata kizazi cha tatu. Pia aliwaona wana wa Makiri mwana wa Manase, waliowekwa katika magoti ya Yusufu. 24Yusufu akawambia ndugu zake, “Ninakaribia kufa; lakini kwa hakika Mungu atawajilia na kuwaongoza kutoka katika nchi hii na kuwapeleka katika nch aliyoapa kumpa Ibrahimu, kwa Isaka na kwa Yakobo.” 25Kisha Yusufu akawaapisha watu wa Israeli kwa kiapo. Akasema, “Bila shaka Mungu atawajilia. Wakati huo mtachukuwa mifupa yangu kutoka hapa.” 26Hivyo Yusufu akafa, mwenye miaka 110. Wakampaka dawa na akawekwa katika jeneza huko Misri.
Sala ya Jioni: somo
8Ongea kwa ajili yao wasioweza kuongea, kwa madai ya wote wanaopotea. 9Ongea na uhukumu kwa vipimo vya haki na utetee dai la masikini na watu wahitaji. 10Mke hodari ni nani anaweza kumpata? Thamani yake ni zaidi kuliko vito. 11Moyo wa mume wake humwamini, na hatakuwa masikini. 12Humtendea mambo mema na wala si mabaya siku zote za maisha yake. 13Huchagua sufu na kitani, na hufanya kazi yake ya mikono kwa furaha. 14Yupo kama meli za wafanyabiashara; huleta chakula chake kutoka mbali. 15Huamka wakati wa usiku na kuwapa chakula watu wa kaya yake, na kugawa kazi kwa watumishi wake wa kike. 16Hulifikiria shamba na kulinunua, kwa tunda la mikono yake hupanda shamba la mizabibu. 17Yeye mwenyewe hujivika nguvu na kuimarisha mikono yake. 18Huangalia ni kipi kitaleta faida nzuri kwake; usiku wote taa yake haizimishwi. 19Mikono yake huiweka kwenye mpini wa kisokotea nyuzi na hushikilia kisokotea nyuzi. 20Mkono wake huwafikia watu masikini; mikono yake huwafikia watu wahitaji. 21Haogopi theluji kwa ajili ya kaya yake, kwa maana nyumba yake yote imevika kwa nguo nyekundu. 22Hutengeneza matandiko ya kitanda chake, na huvaa nguo za kitani ya dhambarau safi. 23Mume wake anajulikana malangoni, anapoketi na wazee wa nchi. 24Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza, na naleta mishipi kwa wafanyabiashara. 25Amevaa nguvu na heshima, na wakati ujao huucheka. 26Anafumbua kinywa chake kwa hekima na sheria ya ukarimu ipo kwenye ulimi wake. 27Huangalia njia za nyumba yake na hawezi kula mkate wa uvivu. 28Watoto wake huinuka na kumwita heri na mume wake humsifia, akisema, 29“Wanawake wengi wamefanya vizuri, lakini wewe umewapita wote.” 30Madaha ni udanganyifu, uzuri ni ubatili; bali mwanamke amchaye Yehova, atasifiwa. 31Mpeni tunda la mikono yake na kazi zake zimsifu katika malango.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini wa Kikasisi Flegonti, padri (1938)
- Mfiadini Demetrio (1942)
- Wafiadini Yakobo, padri, Azadani na Abdikio, mashemasi, wa Uajemi (karibu 380)
- Mfiadini wa Kikasisi Gregori V, Patriarki wa Konstantinopoli (1821)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 10 Aprili katika kalenda ya kanisa ni 23 Aprili katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki