Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 23 Aprili

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 23 Aprili 2027

Ijumaa · Juma la 4 la Pasaka

Sikukuu na watakatifu

Ijumaa ya Juma la 4 la Pasaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: nyeupe

Mt. Adalberti, askofu na shahidi · Kumbukumbu ya hiari

Mt. Georgi, shahidi · Kumbukumbu ya hiari

Kufunga na toba

Siku ya toba

Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mdo 13:26–33

26Ndugu, watoto wa ukoo wa Abrahamu, na wale ambao kati yenu mnamwabudu Mungu, ni kwa ajili yetu kwamba ujumbe huu wa ukombozi umetumwa. 27Kwa wale waishio Yerusalemu, na watawala wao, hawakumtambua kwa uhalisia, na wala hawakuutambua ujumbe wa manabii ambao husomwa kila Sabato; kwa hiyo walitimiliza ujumbe wa manabii kwa kumhukumu kifo Yesu. 28Japokuwa hawakupata sababu nzuri kwa kifo ndani yake, walimwomba Pilato amuue. 29Walipomaliza mambo yote yaliyoandikwa kuhusu yeye, walimshusha kutoka mtini na kumlaza kaburini. 30Lakini Mungu alimfufua kutoka wafu. 31Alionekana kwa siku nyingi kwa wale waliokwenda pamoja naye kutoka Galilaya kuelekea Yerusalemu. Watu hawa sasa ni mashahidi wa watu. 32Hivyo tunawaletea habari njema kuhusu ahadi walizopewa mababu zetu. 33Mungu aliweka ahadi hizi kwetu, watoto wao, katika hilo alimfufua Yesu na kumrudisha tena katika uhai. Hili pia liliandikwa katika Zaburi ya pili: 'Wewe ni Mwanangu, leo nimekuwa Baba yako'

Wimbo wa katikati

Zab 2:6–11

6“Mimi mwenyewe nilimpaka mafuta mfalme wa Sayuni, mlima wangu mtakatifu.” 7Nami nitatangaza amri ya Yahwe. Yeye aliniambia, “wewe ni mwanangu! Leo hii nimekuwa baba yako. 8Uniombe, nami nitakupa wewe taifa kwa ajili ya urithi na mikoa ya nchi iliyo bora kwa ajili ya umiliki wako. 9Wewe utawavunja wao kwa fimbo ya chuma; kama vile mtungi wa mfinyanzi, wewe utawavunja wao vipande vipande.” 10Hivyo sasa, ninyi wafalme; mchukue tahadhari; mjirekebishe. 11Mwabuduni Yahwe kwa hofu na mfurahi mkitetemeka.

Injili

Yn 14:1–6

1“Usiruhusu moyo wako kuwa katika mahangaiko. Unamwamini Mungu niamini pia na mimi. 2Katika nyumba ya Baba yangu kuna makazi mengi ya kukaa; kama isingekuwa hivyo, ningekuwa nimekuambia, kwa vile ninakwenda kukuandalia mahali kwa ajili yako. 3Kama nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena kuwakaribisha kwangu, ili mahali nilipo pia nanyi muwepo. 4Mnajua njia mahali ninakoenda.” 5Tomaso alimwambia Yesu, “Bwana, hatujui mahali unakoenda; Je! Tunawezaje kuijua njia? 6Yesu alimwambia, “ Mimi ndiye njia, kweli, na uzima; hakuna awezaye kuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 23 Aprili

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki