Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 22 Aprili

Kalenda ya Kiorthodoksi · 9 Aprili (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 22 Aprili 2027

Alhamisi · Wiki ya 6 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 5

Sikukuu na watakatifu

Mfiadini Eupsikio (362)

Kwaresima Kuu

Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Saa ya 6

Isa 65:8–16

8Yahwe asema hivi, ''Ikiwa kama juisi itapatikana katika nguzo ya zabibu, wakati mmoja ataposema, 'Usihiaribu hiyo, maa kuna uzuri ndani yake; hichi ndicho nitakachokifanya kwa niaba ya watumishi wangu: Sitawaribu wao wote. 9Nitazileta koo kutoka kwa Yakobo, na kutoka Yuda wao ambao watairithi milima yangu. Niliowachagua watairithi aridhi, na watumishi wangu wataishi pale. 10Sharoni itakuwa malisho ya makundi, na bonde la Akori itakuwa sehemu ya kupumzikia ya makundi yangu, kwa watu wangu wanaonitafuta mimi. 11Lakini yeye aliyeachana na Yehwe, anayeusahau mlima wangu mtakatifu, anayeandaa meza kwa bahati ya mungu, na kujaza kikombe cha mvinyo uliochanganywa na miungu inayoitwa Hatama. 12Nitaufikisha mwisho wenu kwa upanga, na wato mtainama chini kwa kuchinjwa, Kwa sababu nilipokuita wewe, haukuitikia; nilipozungumza haukunisikliza. lakini mlifanya yaliyo mabaya katika macho yangu na kuchagua kufanya yasiyo nipendeza mimi.'' 13Bwana Yahwe asema hivi, ''Tazama, mtumishi atakula, lakini atashikwa na njaa; tazama mtumishi wangu atakunywa lakini atakuwa na kiu; tazama mtumishi wangu atashangilia, lakini atatiwa katika aibu. 14Tazama, mtumishi wangu atapiga kelele za furaha kwa sababu ya furaha ya moyo, lakini utalia kwa sababu ya maumivu ya moyo, na mtapiga kelele kwa sababu ya kusagwa kwa roho zenu. 15Nanyi mtaliacha jina lenu nyuma kama laana kwa watu niliowachagua wazungumze; Mimi Bwana Yahwe, Nitakuwa wewe; Nitawaita watumishi wangu kwa jina lingine. 16Yeyote atakaye tamka baraka juu ya nchi atabarikiwa na mimi, Mungu wa kweli. Yeyote achukuae kiapo juu ya nchi anaapa na mimi, Mungu wa kweli, kwa sababu matatizo ya nyuma yatasaulika, maana yatafichwa machoni pangu.

Sala ya Jioni: somo

Mwa 46:1–7

1Israeli akasafiri na yote aliyokuwa nayo na akaja Beersheba. Pale akatoa sadaka kwa Mungu wa Isaka baba yake. 2Mungu akamwambia Israeli katika ndoto usiku, akisema, “Yakobo, Yakobo.” 3Akasema, “Mimi hapa.” Akasema, “Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako. Usiogope kushuka Misri, kwa maana nitakufanya taifa kubwa huko. 4Nitakwenda pamoja nawe huko Misri, Nami nitakupandisha huku tena bila shaka. Na Yusufu akayafunika macho yako kwa mikono wake.” 5Yakobo akainuka kutoka Beersheba. Wana wa Israeli wakamsafirisha Yakobo baba yao, watoto wao, na wake wao, katika mikokotene ambayo Farao alikuwa ameipeleka kuwachukua. 6Wakachukua mifugo yao na mali zao walizokuwa wamezipata katika nchi ya Kanaani. Wakaja Misri, Yakobo na uzao wake wote pamoja naye. 7Akaja Misri pamoja na wanawe na wana wa wanawe, binti zake na wana wa binti zake, na uzao wake wote.

Sala ya Jioni: somo

Mit 23:15–24:5

15Mwanangu, kama moyo wako una busara, basi moyo wangu utafurahi pia; 16sehemu zangu ndani kabisa zitafurahi sana midomo yako inaponena haki. 17Usiruhusu moyo wako kuwahusudu wenye dhambi, lakini endelea kumcha Yehova siku zote. 18Hakika tumaini lako halitaondolewa na siku zako za hapo baadaye. 19Sikia- wewe! - mwanangu, na uwe mwenye busara na uelekeze moyo wako katika njia. 20Usishirikiane pamoja na walevi, au pamoja na walaji wa nyama walafi, 21maana mlevi na mlafi wanakuwa masikini na usingizi utawavika kwa matambara. 22Msikilize baba yako ambaye alikuzaa na usimdharau mama yako wakati akiwa mzee. 23Inunue kweli, lakini usiiuze; nunua hekima, nidhamu, na ufahamu. 24Baba yake mwenye haki atafurahia sana, na yule amzaaye mtoto mwenye busara atamfurahia. 25Mfurahishe baba yako na mama yako na yule aliyekuzaa afurahie. 26Mwanangu, nipe moyo wako na macho yako yachunguze njia zangu. 27Maana malaya ni shimo refu, na mke wa mume mwingine ni kisima chembamba. 28Anavizia kama mnyang'anyi na huongeza idadi ya wadanganyifu miongoni mwa wanadamu. 29Nani mwenye taabu? Nani mwenye huzuni? Nani mwenye mapigano? Nani mwenye malalamiko? Nani mwenye majeraha bila sababu? Nani mwenye macho mekundu? 30Ni wale ambao huzengea kwenye mvinyo, wale wanaojaribu kuchanganya mvinyo. 31Usiutazame mvinyo ukiwa mwekundu, wakati unametameta kwenye kikombe na kutelemka kwa uraini. 32Mwisho wake unauma kama nyoka na sumu yake kama kifutu. 33Macho yako yataona vitu vigeni na moyo wako utatamka vitu vya ukaidi. 34Utakuwa kama anayelala kwenye bahari au anayelala juu ya mlingoti. “ 35Wamenipiga,” utasema, “ lakini sikuumia. Wamenichapa, lakini sikuwa na hisia. Nitaamka lini? Nitatafuta kinywaji kingine.” 24:1Usiwe na husuda kwa wenye ubaya, wala usitamani kuambatana nao, 2kwa sababu mioyo yao inapanga njama za vurugu na midomo ya huongea juu ya madhara. 3Kwa hekima nyumba hujengwa na kwa ufahamu huimarishwa. 4Kwa maarifa vyumba hujazwa vitu vyote vya thamani na utajiri wa kupendeza. 5Shujaa wa hekima ni imara, na mtu wa maarifa huongeza nguvu zake;

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 22 Aprili

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 9 Aprili katika kalenda ya kanisa ni 22 Aprili katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki