Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 7 Februari

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 7 Februari 2027

Jumapili · Juma la 5 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Dominika ya 5 ya Mwaka

Dominika · Rangi ya liturujia: kijani

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Ayu 7:1–4, 6–7

1Je mtu hana kazi ngumu juu ya nchi? Je siku zake si kama siku za mwajiriwa? 2Kama mtumwa atamaniye sana kivuli cha jioni, kama mwajiriwa atafutaye ujira wake - 3hivyo nami nimeumbwa kuvumilia miezi ya taabu; Nami nimepewa taabu - zimeujaza usiku. 4Hapo nilalapo chini, najiuliza mwenyewe, 'Lini nitatoka kitandani na lini usiku utatoweka?' Nimejawa na kujitupa huku na huko hadi mwanzo wa siku. 6Siku zangu zinakimbia kuliko chombo cha kufumia; zinapita bila tumaini. 7Mungu, anakumbuka kwamba maisha yangu ni pumzi tu; jicho langu halitaona mema tena.

Wimbo wa katikati

Zab 147:1–6

1Msifuni Yahwe, kwa maana ni vyema kumwimbia sifa Mungu wetu, ni kuzuri, kusifu kwa faa sana. 2Yahwe huijenga tena Yerusalemu, huwakusanya pamoja watu wa Israeli waliotawanyika. 3Huponya mioyo iliyopondeka na kuganga majeraha yao. 4Huzihesabu nyota, naye huzipa majina zote. 5Ukuu ni wa Bwana wetu na nguvu zake ni za kutisha, ufahamu wake hauwezi kupimika. 6Yahwe huwainua wanyonge, huwashusha chini wenye jeuri.

Somo la pili

1 Kor 9:16–19, 22–23

16Maana ikiwa naihubiri injili, sina sababu ya kujisifu, kwa sababu ni lazima nifanye hivi. Na ole wangu nisipoihubiri injili! 17Kwa maana nikifanya hivi kwa hiari yangu, nina thawabu. Lakini ikiwa si kwa hiari, bado nina jukumu nililopewa kuwa wakili. 18Basi thawabu yangu ni nini? Ya kuwa nihubiripo, nitaitoa injili pasipo gharama na bila kutumia kwa utimilifu wa haki yangu niliyonayo katika Injili. 19Maana japo nimekuwa huru kwa wote, nilifanyika mtumwa wa wote, ili kwamba niweze kuwapata wengi zaidi. 22Kwa walio wanyonge nilikuwa mnyonge, ili niwapate walio wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa baadhi. 23Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya injili, ili nipate kushiriki katika baraka.

Injili

Mk 1:29–39

29Na mara moja baada ya kutoka nje ya sinagogi, waliingia nyumbani mwa Simoni na Andrea wakiwa na Yakobo na Yohana. 30Sasa mama mkwe wa Simoni alikuwa amelala mgonjwa wa homa, na mara moja walimwambia Yesu habari zake. 31Hivyo alikuja, alimshika kwa mkono, na kumwinua juu; homa ikaondoka kwake, na akaanza kuwahudumia. 32Jioni hiyo wakati jua limekwisha zama, walimletea kwake wote waliokuwa wagonjwa, au waliopagawa na pepo. 33Mji wote walikusanyika pamoja katika mlango. 34Aliwaponya wengi waliokuwa wagonjwa wa magonjwa mbalimbali na kutoa pepo wengi, bali hakuruhusu pepo kuongea kwa sababu walimjua. 35Aliamka asubuhi na mapema, wakati ilikuwa bado giza; aliondoka na kwenda mahali pa faragha na aliomba huko. 36Simoni na wote waliokuwa pamoja naye walimtafuta. 37Walimpata na wakamwambia, “Kila mmoja anakutafuta” 38Aliwaambia, “Twendeni mahali pengine, nje katika miji inayozunguka, ili niweze kuhubiri huko pia. Ndiyo sababu nilikuja hapa.” 39Alikwenda akipita Galilaya yote, akihubiri katika masinagogi yao na kukemea pepo.

Watakatifu wa 7 Februari

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki