Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 8 Februari
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 8 Februari 2027
Jumatatu · Juma la 5 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumatatu ya Juma la 5 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Mt. Yeronimo Emiliani, padre · Kumbukumbu ya hiari
Mt. Yosefina Bakhita, bikira · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi. 2Nayo nchi haikuwa na umbo na ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji. Roho wa Mungu alikuwa akielea juu ya uso wa maji. 3Mungu akasema, “na kuwe nuru,” na kulikuwa na nuru. 4Mungu akaona nuru kuwa ni njema. Akaigawa nuru na giza. 5Mungu akaiita nuru “ mchana” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni na asubuhi, siku ya kwanza. 6Mungu akasema, “ na kuwe na anga kati ya maji, na ligawe maji na maji.” 7Mungu akafanya anga na kugawanya maji yaliyo kuwa chini ya anga na maji ambayo yalikuwa juu ya anga. Ikawa hivyo. 8Mungu akaita anga “mbingu.” Ikawa jioni na asubuhi siku ya pili. 9Mungu akasema, “maji yaliyo chini ya mbingu yakusanyike pamoja mahali pamoja, na ardhi kavu ionekane.” Ikawa hivyo. 10Mungu aliita ardhi kavu “nchi,” na maji yaliyo kusanyika akayaita “bahari.” Akaona kuwa ni vyema. 11Mungu akasema, nchi ichipushe mimea: miche itoayo mbegu na miti ya matunda itoayo matunda ambayo mbegu yake imo ndani ya tunda, kila kitu kwa namna yake.” Ikawa hivyo. 12Nchi ikatoa mimea, miche itoayo mbegu ya aina yake, na miti itoayo tunda ambalo mbegu yake imo ndani yake, kwa aina yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. 13Ikawa jioni na asubuhi, siku ya tatu. 14Mungu akasema, “kuwe na mianga katika anga kutenganisha mchana na usiku. Na ziwe kama ishara, kwa majira, kwa siku na miaka. 15Ziwe mianga katika anga ili kutoa mwanga juu ya nchi.” Ikawa hivyo. 16Mungu akafanya mianga mikuu miwili, mwanga mkuu zaidi kutawala mchana, na mwanga mdogo kutawala usiku. Akafanya nyota pia. 17Mungu akazipanga katika anga kutoa mwanga juu nchi, 18kutawala mchana na usiku, na kugawanya mwanga kutoka kwenye giza. Mungu akaona kuwa ni vyema. 19Ikawa jioni na asubuhi, siku ya nne.
Wimbo wa katikati
Zab 104:1–2, 5–6, 10–12, 24, 35
1Nitamsifu Yahwe maisha yangu yote, Ewe Yahwe Mungu wangu, wewe ni mkubwa sana; umevikwa kwa utukufu na enzi. 2Unajifunika mwenyewe kwa nuru kama kwa mavazi; umetandaza mbingu kama pazia za hema. 5Aliiweka misingi ya nchi, nayo haitahamishwa kamwe. 6Wewe uliifunika nchi kwa maji kama kwa mavazi; maji yalifunika milima. 10Yeye alifanya chemchemi kutiririsha maji mabondeni; mito kutiririka katikati ya milima. 11Inasambaza maji kwa ajili ya wanyama wote wa shambani; punda wa porini hukata kiu yao. 12Kandokando ya mito ndege hujenga viota vyao; huimba kati ya matawi. 24Yahwe, ni jinsi gani kazi zako zilivyo nyingi na za aina mbalimbali! Kwa hekima ulizifanya zote; nchi inafurika kwa kazi zako. 35Wenye dhambi na waondoshwe katika nchi, na waovu wasiwepo tena. Ninamsifu Yahwe maisha yangu yote. Msifuni Yahwe.
Injili
53Nao walipovuka ng'ambo, walifika nchi ya Genesareti mashua ikatia nanga. 54Walipotoka nje ya mashua, mara wakamtambua. 55Wakakimbia kutangaza katika mkoa mzima na wakaanza kuwaleta wagonjwa kwa machela, kila waliposikia anakuja. 56Popote alipoingia katika vijiji, au mjini, au katika nchi, waliwaweka wagonjwa mahali pa soko, na wakamsihi awaruhusu kugusa pindo la vazi lake. Na wote waliomgusa waliponywa.
Watakatifu wa siku
- Mt. Yeronimo Emiliani, padre
- Mt. Yosefina Bakhita, bikira
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki