Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 15 Machi
Kalenda ya Kiorthodoksi · 2 Machi (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 15 Machi 2027
Jumatatu · Wiki ya 1 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 8
Sikukuu na watakatifu
Mwanzo wa Kwaresima Kuu
Kwaresima Kuu
Kujizuia kabisa na chakula
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Saa ya 6
1Maono ya Isaya mtoto wa Amozi ambayo aliyaona kuhusu Yuda na Yerusalemu katika vipindi vya utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda. 2Sikia enyi mbingu, tega sikio ewe nchi; kwa kuwa Yahwe amesema: ''Nimewatunza na kuwalea watoto, lakini wamenigeuka. 3Ng'ombe anamjua anayemmiliki na punda anajua sehemu anapowekewa chakula, lakini Israeli hawajui, wala hawafahamu.'' 4Ole! Taifa, wenye zambi, mtu muovu, watoto wa wenye zambi, watoto wanaoenda kinyume, Wamemtelekeza Yahwe, wamedharau aliye Mtakatifu wa Israeli, wamejitenga wenyew kutoka kwake. 5Kwa nini ulikuwa unaendelea kupigwa? Kwa nini unazidi kuasi zaudi na zaidi? Kichwa chote kinauma, moyo wote ni dhaifu. 6Kutoka kwenye unyayo wa mguu mpaka kichwani kila sehemu ina maumivu; ni madonda na majeraha mabichi yaliyoachwa wazi, ambayo hayajafungwa, kuasifishwa, kuwafunga vidonda vyao, wala kuwaponya kwa mafuta. 7Nchi yenu imeharibiwa; miji yenu imechomwa moto; mashamba yenu— mbele, wageni wamehiaribu; wamepatelekeza katika uharibifu, ulioangushwa na wageni 8Binti Sayuni ameacha kama kibanda katika shamba la mzabu, kama kivuli kitika shamba la matango, kama mji unaomba. 9Kama Yahwe wa majeshi hakutuasha kwa mda mfupi tungekuwa kama Sodoma, tungekuwa kama Gomora. 10Sikiliza neno la Yahwe, enyi viongozi wa Sodomu; sikilizeni sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora: 11''Sadaka zenu ni nyingi kiasi gani kwangu?'' asema Yahwe. ''Nimesikia vya kutosha kuhusu sadaka yenu ya mwana kondoo, na mnyama alionona; na damu ya ng'ombe, ndama, au mbuzi si vifurahii. 12Ulipokuja kuonekaa mbele yangu, Ni nani aliyehitaji hili juu yako, kukanyaga katika mahama yangu 13Msilete tena sadaka zisizo na maana; maana zinaniongezea uchafu mmekusanyika katika siku yenu mpya ya mwenzi na sabato—Mimi siwezi vumlia mikusanyio hii ya waovu. 14Ninaichukia sherehe yenu mpya ya mwenzi na sherehe zilizoteuliwa; ni mzigo kwangu; nimechoka kuubeba. 15Hivyo basi mnapotawanya mikono yenu kitkika maombi, sitawangalia hata kama mkiomba sana, sitawasikiliza; mikono yenu imejaa damu. 16Jiosheni, jitakaseni wenyewe; ondoeni matendo maovu mbele ya macho yangu; acheni kutenda dhambi; 17jifunze kutenda mema; tafuta ukweli; msiwanyanyase, wapeni haki yatima, walindeni wajane.'' 18Njooni sasa, njooni tusemezane, asema Yahwe, japokuwa dhambi zenu ni nyekundu kama bendera zitakuwa nyeupe kama theluji; japokuwa ni myekundu kama damu zitakuwa kama sufi. 19Kama utakubali na kutii, utakula mema ya nchi, 20lakini ukikataa na kugeuka, upanga utakuangamiza, maama Yahwe amesema.
Sala ya Jioni: somo
1Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi. 2Nayo nchi haikuwa na umbo na ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji. Roho wa Mungu alikuwa akielea juu ya uso wa maji. 3Mungu akasema, “na kuwe nuru,” na kulikuwa na nuru. 4Mungu akaona nuru kuwa ni njema. Akaigawa nuru na giza. 5Mungu akaiita nuru “ mchana” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni na asubuhi, siku ya kwanza. 6Mungu akasema, “ na kuwe na anga kati ya maji, na ligawe maji na maji.” 7Mungu akafanya anga na kugawanya maji yaliyo kuwa chini ya anga na maji ambayo yalikuwa juu ya anga. Ikawa hivyo. 8Mungu akaita anga “mbingu.” Ikawa jioni na asubuhi siku ya pili. 9Mungu akasema, “maji yaliyo chini ya mbingu yakusanyike pamoja mahali pamoja, na ardhi kavu ionekane.” Ikawa hivyo. 10Mungu aliita ardhi kavu “nchi,” na maji yaliyo kusanyika akayaita “bahari.” Akaona kuwa ni vyema. 11Mungu akasema, nchi ichipushe mimea: miche itoayo mbegu na miti ya matunda itoayo matunda ambayo mbegu yake imo ndani ya tunda, kila kitu kwa namna yake.” Ikawa hivyo. 12Nchi ikatoa mimea, miche itoayo mbegu ya aina yake, na miti itoayo tunda ambalo mbegu yake imo ndani yake, kwa aina yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. 13Ikawa jioni na asubuhi, siku ya tatu.
Sala ya Jioni: somo
1Mithali za Sulemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli. 2Mithali hizi zinafundisha hekima na maarifa, kufundisha maneno ya busara, 3ili mpate maarifa kwa ajili ya kuishi kwa kutenda wema, haki na adili. 4Mithali hizi zinatoa hekima kwa wale ambao hawakufunzwa, na kuwapa vijana maarifa na hadhari. 5Watu wenye busara wasikie na kuongeza elimu yao na watu wenye ufahamu wapate mwongozo, 6kwa kuelewa mithali, misemo, vitendawili na maneno ya wenye busara. 7Hofu ya Yehova ni chanzo cha maarifa- wapumbavu hudharau hekima na nidhamu. 8Mwanangu, sikia fundisho la baba yako na wala usiziache kanuni za mama yako; 9zitakuwa kilemba cha neema katika kichwa chako na jebu zinazoning'inia kwenye shingo yako. 10Mwanangu wenye dhambi wakikushawishi katika dhambi zao, kataa kuwafuata. 11Kama watasema, “ haya tufuatae, tuvizie ili kufanya mauaji, tujifiche ili tuwashambulie watu wasio na hatia, pasipo sababu. 12Haya tuwameza wakiwa hai, kama kuzimu inavyowachukua wenye afya, na kuwa kama wale waangukao kwenye shimoni. 13Tutapata vitu vyote vya thamani; tutazijaza nyumba zetu vile tunavyoiba kwa wengine. 14Weka vitu vyako kwetu; tutakuwa na mfuko moja kwa pamoja.” 15Mwanangu, usitembee katika njia moja pamoja nao; usiruhusu mguu wako kugusa katika mapito yao; 16miguu ya hukimbilia mabaya na huharakisha kumwaga damu. 17Kwa kuwa haina maana kumtegea ndege mtego wakati ndege anaona. 18Watu hawa huvizia kujiua wenyewe—wanatega mtego kwa ajili yao wenyewe. 19Ndivyo zilivyo njia za kila ambaye hupata utajiri kwa udhalimu; mapato ya udhalimu huondoa uhai wa wenye utajiri. 20Hekima inalia kwa sauti mtaani, inapaza sauti katika viwanja;
Watakatifu wa siku
- Ikoni ya Mama wa Mungu iitwayo “Mtawala” (1917)
- Mfiadini wa Kikasisi Theodoto, Askofu wa Kirenia (karibu 326)
- Askofu Mtakatifu Arsenio, Askofu wa Tver (1409)
- Mfiadini Euthalia (257)
- Mfiadini Troadio (karne ya 3)
- Mtakatifu Mtawa Agatho wa Misri (karne ya 5)
- Wafiadini 440 wa Italia (579)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 2 Machi katika kalenda ya kanisa ni 15 Machi katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki