22Mara moja aliwaamuru wanafunzi waingie ndani ya mashua, wakati huo yeye akawaaga umati waende zao.
23Baada ya kuwaaga umati kwenda zao, akapanda juu mlimani kuomba pekee yake. Wakati ilipokuwa jioni alikuwa huko pekee yake.
24Lakini sasa mashua ilipokuwa katikati ya bahari ukiyumbayumba kwa sababu ya mawimbi, kwani upepo ulikuwa wa mpisho.
25Katika usiku wa zamu ya nne Yesu aliwakaribia, akitembea juu ya maji.
26Wakati wanafunzi wake walipomwona akiitembea juu ya bahari, walihofu na kusema, “Ni mzuka,'' na kupaaza sauti katika hali ya uoga.
27Yesu akawaambia mara moja, akisema, “Jipeni moyo! ni mimi! msiogope.”
28Petro alimjibu kwa kusema, “Bwana, kama ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.''
29Yesu akasema, “Njoo.'' Hivyo Petro akatoka ndani ya mashua na akatembea juu ya maji kwenda kwa Yesu.
30Lakini Petro alipoona mawimbi, aliogopa, na kuanza kuzama, chini, akaita sauti na kusema, “Bwana, niokoe!''
31Haraka Yesu akanyoosha mkono wake akamnyanyua Petro, na kumwambia, “Wewe mwenye imani ndogo, kwa nini ulikuwa na mashaka?”
32Ndipo Yesu na Petro walipoingia katika mashua, upepo ulikoma kuvuma.
33Wanafunzi mashuani wakamwabudu Yesu na kusema, “Kweli wewe ni Mwana wa Mungu.”