Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Katika Galilaya

Injili kando kwa kando · Katika Galilaya

Wale Kumi na Wawili watumwa

Mt 10:5–15 · Mk 6:7–13 · Lk 9:1–6

Mathayo

Mt 10:5–15

5Hawa kumi na wawili Yesu aliwatuma. Naye aliwaelekeza akisema “Msiende sehemu wanakoishi wamataifa na msiingie kwenye miji ya wasamalia.

6Badala yake, mwende kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israel.

7Na mnapokwenda, hubirini na kusema, ufalme wa mbinguni umekaribia.'

8Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma na fukuzeni pepo. Mmepokea bure, toeni bure.

9Msichue dhahabu, almasi au shaba kwenye pochi zenu.

10Usichukue mkoba katika safari yenu, au nguo za ziada, viatu au fimbo, kwa kuwa mfanyakazi anastahili chakula chake.

11Mji wowote au kijiji mtakachoingia, tafuteni ambaye anastahili na mkae pale mpaka mtakapoondoka.

12Mtakapoingia katika nyumba salimieni,

13endapo nyumba inastahili, amani yenu ibaki pale, lakini kama nyumba haistahili, amani yenu iondoke pamoja nanyi.

14Na kwa wale wasiowapokea ninyi au kusikiliza maneno yenu, wakati mnaondoka kwenye nyumba au mji huo, jipanguseni mavumbi ya nyayo zenu mahali hapo.

15Kweli ninawaambia, itakuwa ya kustahimili zaidi miji ya Sodoma na Gomorah siku ya hukumu kuliko mji huo.

Marko

Mk 6:7–13

7Aliwaita wale wanafunzi kumi na wawili akaanza kuwatuma wawili wawili. Aliwapa mamlaka juu ya pepo wachafu,

8na kuwaamuru wasichukue chochote wanapokwenda isipokuwa fimbo tu. Wasichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kibindoni;

9lakini wavae viatu, na siyo kanzu mbili.

10Na akawaambia, “Nyumba yoyote mtakayoingia, kaeni hapo mpaka mtakapoondoka.

11Na mji wowote usipowapokea wala kuwasikiliza, ondokeni kwao, kung'uteni mavumbi ya miguu yenu, iwe ushuhuda kwao.”

12Nao wakaenda wakitangaza watu watubu na kuacha dhambi zao.

13Waliwafukuza pepo wengi, na waliwapaka mafuta wagonjwa na wakaponywa.

Luka

Lk 9:1–6

1Akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa uwezo na mamlaka juu ya mapepo yote na kuponya magonjwa.

2Akawatuma waende kuhubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.

3Akawaambia, “Msichukue chochote kwa ajili ya safari yenu wala fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala pesa wala msichukue kanzu mbili.

4Nyumba yoyote mtakayo iingia, kaeni humo mpaka mtakapo ondoka mahali hapo.

5Na kwa wale wasio wapokea, mtakapo ondoka mji huo, jikung'uteni vumbi katika miguu yenu kwa ushuhuda juu yao”.

6Wakaondoka na kwenda kupitia vijijini, wakitangaza habari njema na kuponya watu kila mahali.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY