1Kwa wakati huo, Herode alisikia habari juu ya Yesu..
2Akawaambia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka katika wafu. Kwa hiyo nguvu hizi zipo juu yake.”
3Kwa kuwa Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumtupa gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo kaka yake.
4Kwa kuwa Yohana alimwambia, “Si halali kumchukua yeye kuwa mke wake.”
5Herode angemwua lakini aliwaogopa watu kwa sababu walimwona Yohana kuwa nabii.
6Lakini wakati siku ya kuzaliwa Herode ilipofika binti wa Herodia alicheza katikati ya watu na kumpendeza Herode.
7Katika kujibu kili aliahidi kwa kiapo kwamba atampa chochote atakachoomba.
8Baada ya kushauriwa na mama yake, alisema, “Nipe mimi hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.”
9Mfalme alikuwa na sikitiko kwa maombi ya binti, lakini kwa ajili ya kiapo chake, kwa sababu ya wote waliokuwa chakulani pamoja naye aliamuru kwamba inapaswa ifanyike.
10Alituma Yohana aletwe kutoka gerezani
11ili akatwe kichwa chake na kikaletwa juu ya sinia na akapewa binti na akakipeleka kwa mama yake.
12Kisha wanafunzi wake wakaja kuuchukua ule mwili na kuuzika, baada ya hili walienda kumwambia Yesu.