1Yesu akaingia kwenye boti, akavuka na akafika kwenye mji alipokuwa anaishi.
2Tazama, wakamletea mtu aliyepooza amelazwa kwenye godoro. alipooiona imani yao, Yesu akamwambia mtu aliyepooza, “Mwanangu, uwe na furaha, Dhambi zako zimesamehewa”
3Tazama, Baadhi ya walimu wa sheria wakasemezana wao kwa wao, “Huyu mtu anakufuru”
4Yesu akatambua mawazo yao na kusema, “Kwa nini mnawaza maovu moyoni mwenu?
5Kipi kilicho rahisi kusema, 'Dhambi zako zimesamehewa' au kusema, 'Simama na utembee?'
6Lakini mtambue ya kwamba Mwana wa Adamu anao uwezo wa kusamehe dhambi...” aliyasema haya kwa yule aliyepooza, “Simama, chukua godoro lako, na uende nyumbani kwako”
7Ndipo yule mtu akasimama na kuondoka kwenda nyumbani kwake.
8Makutano walipoona hayo, walishangaa na kumsifu Mungu, ambaye amewapa uwezo huo watu.