57Ilipofika jioni, alikuja mtu tajiri kutoka Arimathayo, aliyeitwa Yusufu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu.
58Alimwendea Pilato na kuuomba mwili wa Yesu. Kisha Pilato aliagiza apate kupewa.
59Yusufu aliuchukua mwili akaufunga na nguo ya sufi safi,
60na akaulaza katika kaburi jipya lake alilokuwa amelichonga mwambani. Kisha akavingirisha jiwe kubwa likafunika mlango wa kaburi na akaenda zake.
61Mariamu Magdalena na Mariamu mwingine walikuwa pale, wamekaa kuelekea kaburi.