45Sasa kutoka saa sita kulikuwa na giza katika nchi yote hadi saa tisa.
46Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu, “Eloi, Eloi, lama thabakithan?” akimaanisha, “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?”
47Wakati huo baadhi yao waliokuwa wamesimama pale walisikia, wakasema, “Anamwita Eliya.”
48Mara moja mmoja wao alikimbia kuchukua sifongo na kuijaza kinywaji kichungu, akaiweka juu ya mti na kumpa apate kunywa.
49Nao waliosalia wakasema, “Mwacheni peke yake, acheni tuone kama Eliya atakuja kumwokoa.”
50Kisha Yesu akalia tena kwa sauti kuu na akaitoa roho yake.
51Tazama, Pazia la hekalu lilipasuka sehemu mbili kutokea juu hadi chini. Na ardhi ikatetemeka na miamba ikapasuka vipande.
52Makaburi yalifunguka, na miili ya watakatifu wengi waliokuwa wamelala usingizi walifufuliwa.
53Walitoka kwenye makaburi baada ya ufufuo wake, waliingia mji mtakatifu, na wakaonekana na wengi.
54Basi yule akida na wale ambao walikuwa wakimtazama Yesu waliona tetemeko na mambo yaliyokuwa yakitokea, walijawa na woga sana na kusema, “Kweli huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”
55Wanawake wengi waliokuwa wakimfuata Yesu kutoka Galilaya ili kumhudumia walikuwa pale wakitazama kutoka kwa mbali.
56Miongini mwao walikuwa Mariamu Magdarena, Mariamu mama yake Yakobo na Joseph, na mama wa watoto wa Zebedayo