Mwanzo › Biblia inasema nini › Majaribu
Nyakati ngumu
Biblia inasema nini kuhusu Majaribu
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (12), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
1 Kor 10:13
Hakuna jaribu lililowapata ninyi lisilo kawaida ya wanadamu. Ila Mungu ni mwaminifu. Hatawaacha mjaribiwe kupita uwezo wenu. Pamoja na jaribu yeye atawapa mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.Mt 26:41
Kesheni na kuomba kusudi msiingie majaribuni. Roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.”Yak 4:7
Hivyo, jitoeni kwa Mungu. Mpingeni ibilisi na yeye atakimbia kutoka kwenu.Ebr 2:18
Kwa sababu Yesu mwenyewe ameteseka, na kujaribiwa, ana uwezo wa kuwasaidia wale wanaojaribiwa.Mt 6:13
Na usitulete katika majaribu, lakini utuepushe kutoka kwa yule mwovu.'Efe 6:11
Vaeni silaha zote za Mungu, ili kwamba mpate kusimama kinyume na hila za shetani.Yak 1:12
Amebarikiwa mtu yule anayevumilia majaribu, kwa kuwa baada ya kushinda jaribu hilo, atapokea taji ya uzima, ambayo imeahidiwa kwa wale wampendao Mungu.Lk 22:40
Walipofika, aliwaambia, “Ombeni kwamba msiingie majaribuni.”1 Tim 6:9
Sasa hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu, katika mtego. Huanguka katika upumbavu mwingi na tamaa mbaya, na katika kitu chochote kinachowafanya watu wazame katika maangamizi na uharibifu.1 Kor 6:18
Ikimbieni zinaa! “Kila dhambi aifanyayo mtu ni nje na mwili wake. Lakini zinaa, mtu hutenda dhambi dhidi ya mwili wake mwenyewe.Ebr 4:15
Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu ambaye hawezi kuhisi huruma kwa ajili udhaifu wetu, lakini yeye ambaye kwa njia zote amekuwa akijaribiwa kama sisi, isipokuwa yeye ambaye hana dhambi.Mk 14:38
Kesheni na muombe kwamba msije mkaingia katika majaribu. Hakika roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.”Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0