Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Dhiki na nyakati ngumu

Nyakati ngumu

Biblia inasema nini kuhusu Dhiki na nyakati ngumu

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (12), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Yak 1:2–4Hesabuni kuwa ni furaha zaidi, ndugu zangu, mnapopita katika matatizo mbali mbali, mkijua kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huwapa uvumilivu. Acheni uvumilivu uikamilishe kazi yake, kwamba muweze kukomaa kikamilifu, bila kupungukiwa katika lolote.
Isa 41:10Usiogope maana mimi niko pamoja na wewe. Usiwe na wasiwasi, maana mimi ni Mungu wako. Nitakutia nguvu, na nitakusaidia, wewe, na Nitakushika kwa mkono wa haki yangu.
Yn 16:33Nawaambia mambo haya ili kwamba ndani yangu muwe na amani. Duniani mna matatizo, lakini jipeni moyo, nimeushinda ulimwengu.
Rum 8:18Kwa kuwa nayahesabu mateso ya wakati huu kuwa si kitu nikilinganisha na utukufu utakaofunuliwa kwetu.
Yak 1:12Amebarikiwa mtu yule anayevumilia majaribu, kwa kuwa baada ya kushinda jaribu hilo, atapokea taji ya uzima, ambayo imeahidiwa kwa wale wampendao Mungu.
Rum 5:3–5Siyo hili tu, lakini pia tunafurahi katika mateso yetu. Tunajua kwamba mateso huzaa uvumilivu. Uvumilivu huzaa kukubalika, na kukubalika huzaa ujasiri kwa ajili ya baadaye. Ujasiri huu haukatishi tamaa, kwa sababu upendo wa Mungu umemwagwa katika mioyo yetu kupitia Roho Mtakatifu, ambaye alitolewa kwetu.
Yos 1:9Je si mimi niliyekuagiza? Uwe hadori na jasiri! Usiogope. Usivunjike moyo. Yahweh Mungu wako yuko pamoja nawe kila uendeko.
Rum 8:28Nasi twajua ya kuwa kwa wote wampendao Mungu, yeye hufanya mambo yote pamoja kwa wema, kwa wale wote walioitwa kwa kusudi lake.
1 Pet 4:12–13Wapendwa, msihesabu jaribu ambalo huja kuwajaribu kama kitu kigeni, ingawa kuna kitu kigeni kilichokuwa kinatukia kwenu. Lakini kwa kadri mnavyozidi kupata uzoefu wa mateso ya Kristo, furahini, ili kwamba mfurahi pia na kushangilia katika ufunuo wa utukufu wake.
Yer 29:11–13Kwa maana mimi mwenyewe naijua mipangao niliyonayo kwa ajili yenu—hili ni tangazo la Yahwe—mipango kwa ajili ya amani na siyo kwa ajili ya mabaya, ili kuwapa ninyi tumaini na siku zenu za mwisho. Kisha mtaniita, na kwenda na kuniomba mimi, na nitawasikiliza. Kwa maana mtanitafuta na kunipata, kwa kuwa mtanitafuta kwa moyo wenu wote.
Flp 4:13Ninaweza kufanya haya kwa kuwezeshwa na Yeye anitiaye nguvu.
Zab 9:9–10Yahweh pia atakuwa ngome kwake aliye onewa, na ngome wakati wa shida. Wale wakujuao jina lako wanaamini katika Wewe, kwa ajili yako, Yahweh, usiwaache wale wakutafutao.

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0