Mwanzo › Biblia inasema nini › Nguvu
Nyakati ngumu
Biblia inasema nini kuhusu Nguvu
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Isa 40:31
Lakini wale watakao mngojea Yahwe watapewa nguvu mpya; na watapaa kwa mbawa kama malaika; watakimbia wala hawatachoka; watatembea wala hawatazimia.Flp 4:13
Ninaweza kufanya haya kwa kuwezeshwa na Yeye anitiaye nguvu.Zab 18:32–34
Ni Mungu anitiaye nguvu ndani yangu kama vile mkanda, ambaye humweka mtu mwenye lawama katika njia yake. Yeye hunifanya miguu yangu kuwa myepesi kama mbawala na kuniweka mahali pa juu! Yeye hufunza viganja vyangu kwa ajili ya vita na mikono yangu kupiga upinde wa shaba.Hab 3:19
Bwana Yahwe ni nguvu yangu na anaifanya miguu yangu kama ya kulungu. Ananifanya mimi niende mbele mahali pangu pa juu. - kufuata maelekezo ya muziki, katika vyombo vyangu vya nyuzi.Isa 41:10
Usiogope maana mimi niko pamoja na wewe. Usiwe na wasiwasi, maana mimi ni Mungu wako. Nitakutia nguvu, na nitakusaidia, wewe, na Nitakushika kwa mkono wa haki yangu.1 Nya 22:13
Kisha utafanikiwa, kama tu ukitii maagizo na amri Yahweh alizo mpa Musa kuhusu Israeli. Kuwa hodari na mshujaa. Usiogope wala kufadhaika.Efe 6:10
Hatimaye, iweni na nguvu katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake.Zab 73:26
Mwili wangu na moyo wangu huwa dhaifu, bali Mungu ndiye nguvu ya moyo wangu daima.1 Nya 16:11
Mtafute Yahweh na nguvu zake; tafuteni uwepo wake siku zote.Kum 31:6
Uwe hodari na mwenye ujasiri mwema, usiogope, na usiwaogope; kwa maana Yahwe Mungu wako, ni yeye aendaye kabla yako; hatakuangusha wala kukuacha.”Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0