Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Kuteseka

Nyakati ngumu

Biblia inasema nini kuhusu Kuteseka

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Rum 8:18Kwa kuwa nayahesabu mateso ya wakati huu kuwa si kitu nikilinganisha na utukufu utakaofunuliwa kwetu.
Ufu 21:4Atafuta kila chozi kutoka katika macho yao, na hapatakuwa na kifo tena, au kuomboleza, au kulia, au maumivu. Mambo ya zamani yamekwishakupita.
Rum 5:3–5Siyo hili tu, lakini pia tunafurahi katika mateso yetu. Tunajua kwamba mateso huzaa uvumilivu. Uvumilivu huzaa kukubalika, na kukubalika huzaa ujasiri kwa ajili ya baadaye. Ujasiri huu haukatishi tamaa, kwa sababu upendo wa Mungu umemwagwa katika mioyo yetu kupitia Roho Mtakatifu, ambaye alitolewa kwetu.
Yak 1:2–4Hesabuni kuwa ni furaha zaidi, ndugu zangu, mnapopita katika matatizo mbali mbali, mkijua kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huwapa uvumilivu. Acheni uvumilivu uikamilishe kazi yake, kwamba muweze kukomaa kikamilifu, bila kupungukiwa katika lolote.
2 Kor 4:17Kwa kipindi hiki kifupi, mateso haya mepesi yanatuandaa sisi kwa ajili ya umilele mzito wa utukufu uzidio vipimo vyote.
Zab 41:3Awapo kwenye kitanda cha mateso Yahwe atamsaidia; nawe utakifanya kitanda cha ugonjwa kuwa kitanda cha uponyaji.
Ayu 30:17Mifupa inauma ndani yangu wakati wa usiku; maumivu yanayonisaga hayaishi.
1 Pet 5:10Baada ya kuteseka kwa muda kitambo, Mungu wa neema yote, aliyewaita katika utukufu wa milele ndani ya Kristo, atawakamilisha, atawaimarisha na kuwatia nguvu.
1 Pet 4:12–13Wapendwa, msihesabu jaribu ambalo huja kuwajaribu kama kitu kigeni, ingawa kuna kitu kigeni kilichokuwa kinatukia kwenu. Lakini kwa kadri mnavyozidi kupata uzoefu wa mateso ya Kristo, furahini, ili kwamba mfurahi pia na kushangilia katika ufunuo wa utukufu wake.
Zab 34:19Mateso ya wenye haki ni mengi, bali Yahwe huwaokoa nayo yote.

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0